2 Wakorintho 8:1-3
2 Wakorintho 8:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Ndugu, tunapenda kuwapa habari juu ya neema ambazo Mungu ameyajalia makanisa ya Makedonia. Waumini wa huko walijaribiwa sana kwa taabu; lakini furaha yao ilikuwa kubwa hivi hata wakawa wakarimu kupita kiasi, ingawaje walikuwa maskini sana. Naweza kushuhudia kwamba walikuwa wakarimu kadiri ya nguvu zao na hata zaidi. Kwa hiari yao wenyewe
2 Wakorintho 8:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia; maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao. Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao
2 Wakorintho 8:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tena ndugu zetu, twawaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia; maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao. Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao
2 Wakorintho 8:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Basi sasa ndugu, nataka ninyi mjue kuhusu ile neema ambayo Mungu amewapa makanisa ya Makedonia. Ingawa walikuwa na majaribu makali, furaha yao kubwa na umaskini wao mkuu zilifurika kwa ukarimu mwingi. Kwa maana nashuhudia kwamba wao walitoa kwa kadiri walivyoweza, hata na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao