2 Wakorintho 7:2-4
2 Wakorintho 7:2-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Tunaomba mtupe nafasi mioyoni mwenu! Hatujamkosea mtu yeyote, hatujamdhuru wala kumdanganya mtu yeyote. Sisemi mambo haya kwa ajili ya kumhukumu mtu; maana, kama nilivyokwisha sema, nyinyi mko mioyoni mwetu, tufe pamoja, tuishi pamoja. Nina imani kubwa sana ninaposema nanyi; naona fahari kubwa juu yenu! Katika taabu zetu nimepata kitulizo kikubwa na kufurahi mno.
2 Wakorintho 7:2-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu yeyote, wala kumharibu mtu, wala kumkosea mtu. Sisemi neno hilo ili niwahukumu ninyi kuwa na hatia; kwa maana nimetangulia kusema, ya kwamba ninyi mmo mioyoni mwetu hata kwa kufa pamoja, na kuishi pamoja. Ninao ujasiri mwingi kwenu; naona fahari kuu juu yenu. Nimejaa faraja, katika dhiki yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi.
2 Wakorintho 7:2-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tupeni nafasi mioyoni mwenu. Hatukumdhulumu mtu ye yote, wala kumharibu mtu, wala kumkaramkia mtu. Sisemi neno hilo ili niwahukumu ninyi kuwa na hatia; kwa maana nimetangulia kusema, ya kwamba ninyi mmo mioyoni mwetu hata kwa kufa pamoja, na kuishi pamoja. Ninao ujasiri mwingi kwenu; naona fahari kuu juu yenu. Nimejaa faraja, katika dhiki yetu yote nimejaa furaha ya kupita kiasi.
2 Wakorintho 7:2-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Tupatieni nafasi mioyoni mwenu. Hatujamkosea mtu yeyote, wala hatujampotosha mtu yeyote, wala hatujamdhulumu mtu yeyote. Sisemi haya ili kuwahukumu, kwa kuwa nilisema mwanzo kwamba ninyi mko mioyoni mwetu hata kwa kufa pamoja au kuishi pamoja. Nina ujasiri mwingi kwa ajili yenu; naona fahari juu yenu. Nimejawa na faraja. Nina furaha kupita kiasi katika mateso yetu yote.