2 Wakorintho 5:7-9
2 Wakorintho 5:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana tunaishi kwa imani, na si kwa kuona. Lakini tuko imara na tungependelea hata kuyahama makao haya, tukahamie kwa Bwana. Lakini jambo la maana zaidi, tunataka kumpendeza, iwe tunaishi hapa duniani au huko.
2 Wakorintho 5:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
(Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.) Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwemo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana. Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye.
2 Wakorintho 5:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
(Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.) Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana. Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye.
2 Wakorintho 5:7-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona. Naam, tuna ujasiri, na tunaona ingekuwa bora zaidi kuuacha mwili huu na kwenda kukaa na Bwana. Kwa hiyo, tukiwa katika mwili huu au tukiwa mbali nao, lengo letu ni kumpendeza Bwana.