2 Wakorintho 5:6-8
2 Wakorintho 5:6-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Tuko imara daima. Tunajua kwamba kuishi katika mwili huu tu ni kukaa mbali na Bwana. Maana tunaishi kwa imani, na si kwa kuona. Lakini tuko imara na tungependelea hata kuyahama makao haya, tukahamie kwa Bwana.
2 Wakorintho 5:6-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana. (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.) Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwemo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana.
2 Wakorintho 5:6-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana. (Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.) Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana.
2 Wakorintho 5:6-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa hiyo siku zote tuna ujasiri, hata ingawa tunajua kwamba tukiwa katika mwili huu, tuko mbali na Bwana. Kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona. Naam, tuna ujasiri, na tunaona ingekuwa bora zaidi kuuacha mwili huu na kwenda kukaa na Bwana.