2 Wakorintho 12:1-3,7
2 Wakorintho 12:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Nitajivuna basi, ingawa haifai! Lakini sasa nitasema juu ya maono na ufunuo alivyonijalia Bwana. Namjua mtu mmoja Mkristo, ambaye miaka kumi na minne iliyopita alinyakuliwa mpaka katika mbingu ya tatu. (Sijui kama alikuwa huko kwa mwili au kwa roho; Mungu ajua). Narudia: Najua kwamba mtu huyo alinyakuliwa mpaka peponi. (Lakini sijui kama alikuwa huko kwa mwili au kwa roho; Mungu ajua).
2 Wakorintho 12:7 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini, kusudi mambo haya makuu niliyofunuliwa yasinifanye nilewe majivuno, nilipewa maumivu mwilini kama mwiba, mjumbe wa Shetani mwenye kunipiga, nisijivune kupita kiasi.
2 Wakorintho 12:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikia maono na mafunuo ya Bwana. Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua)
2 Wakorintho 12:7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nilipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.
2 Wakorintho 12:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sina budi kujisifu, ijapokuwa haipendezi; lakini nitafikilia maono na mafunuo ya Bwana. Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu. Nami namjua mtu huyo, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua)
2 Kor 12:7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na makusudi nisipate kujivuna kupita kiasi, kwa wingi wa mafunuo hayo nalipewa mwiba katika mwili, mjumbe wa Shetani ili anipige, nisije nikajivuna kupita kiasi.
2 Wakorintho 12:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Yanipasa nijisifu. Ingawa haifaidi kitu, nitanena kuhusu maono na mafunuo kutoka kwa Bwana. Namjua mtu mmoja katika Kristo ambaye miaka kumi na nne iliyopita alichukuliwa juu hadi mbingu ya tatu. Kama ni katika mwili au nje ya mwili, sijui, Mungu ajua. Nami najua kwamba mtu huyu, iwe ni katika mwili au nje ya mwili mimi sijui, lakini Mungu ajua