Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

2 Mambo ya Nyakati 36:6-7 - Compare All Versions

2 Mambo ya Nyakati 36:6-7 BHN (Biblia Habari Njema)

Nebukadneza mfalme wa Babuloni, alimshambulia, akamfunga kwa pingu ili kumpeleka mateka Babuloni. Nebukadneza pia alitwaa baadhi ya vyombo vya nyumba ya Mwenyezi-Mungu akavipeleka Babuloni na kuviweka katika ikulu yake huko Babuloni.

2 Mambo ya Nyakati 36:6-7 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Juu yake akakwea Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akamfunga kwa pingu, amchukue mpaka Babeli. Nebukadreza akachukua baadhi ya vyombo vya nyumba ya BWANA mpaka Babeli, akavitia katika hekalu lake huko Babeli.

2 Mambo ya Nyakati 36:6-7 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Juu yake akakwea Nebukadneza, mfalme wa Babeli, akamfunga kwa pingu, amchukue mpaka Babeli. Nebukadneza akachukua baadhi ya vyombo vya nyumba ya BWANA mpaka Babeli, akavitia katika hekalu lake huko Babeli.

2 Mambo ya Nyakati 36:6-7 NEN (Neno)

Nebukadneza mfalme wa Babeli akamshambulia na kumfunga kwa pingu za shaba akampeleka Babeli. Nebukadneza akachukua pia vyombo kutoka Hekalu la BWANA na kuviweka katika hekalu lake huko Babeli.