2 Mambo ya Nyakati 20:2-3
2 Mambo ya Nyakati 20:2-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Watu kadhaa walikuja wakamwambia mfalme Yehoshafati, “Jeshi kubwa limekuja kukushambulia kutoka Edomu, ngambo ya Bahari ya Chumvi. Tayari wamekwisha teka Hasason-tamari.” (Hili ni jina lingine la Engedi). Yehoshafati akashikwa na woga, akamwomba Mwenyezi-Mungu amwongoze. Akatangaza watu wote nchini Yuda wafunge.
2 Mambo ya Nyakati 20:2-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng'ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio Engedi). Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute BWANA; akatangaza watu wote kufunga katika Yuda yote.
2 Mambo ya Nyakati 20:2-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng’ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio En-gedi). Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute BWANA; akatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yote.
2 Mambo ya Nyakati 20:2-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Watu fulani wakaja wakamwambia Yehoshafati, “Jeshi kubwa linakuja dhidi yako kutoka Shamu tokea ngʼambo ile nyingine ya Bahari. Tayari liko Hasason-Tamari” (yaani En-Gedi). Yehoshafati akaogopa, akaamua kumtafuta BWANA, na akatangaza kwa Yuda wote kufunga.