2 Mambo ya Nyakati 19:1-2
2 Mambo ya Nyakati 19:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Mfalme Yehoshafati wa Yuda alirejea salama katika ikulu yake mjini Yerusalemu. Lakini mwonaji Yehu mwana wa Hanani, alikwenda kumlaki mfalme, akamwambia, “Je, unadhani ni vema kuwasaidia waovu na kuwapenda wamchukiao Mwenyezi-Mungu? Mambo uliyofanya yamekuletea ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu.
2 Mambo ya Nyakati 19:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Yehoshafati mfalme wa Yuda akarudi Yerusalemu nyumbani kwake kwa amani. Yehu mwana wa Hanani mwonaji akatoka kwenda kumlaki, akamwambia mfalme Yehoshafati, Je! Imekupasa kuwasaidia waovu, na kuwapenda wamchukiao BWANA? Kwa ajili ya hayo ghadhabu itokayo kwa BWANA i juu yako.
2 Mambo ya Nyakati 19:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Yehoshafati mfalme wa Yuda akarudi Yerusalemu nyumbani kwake kwa amani. Yehu mwana wa Hanani mwonaji akatoka kwenda kumlaki, akamwambia mfalme Yehoshafati, Je! Imekupasa kuwasaidia waovu, na kuwapenda wamchukiao BWANA? Kwa ajili ya hayo ghadhabu i juu yako itokayo kwa BWANA.
2 Mambo ya Nyakati 19:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mfalme Yehoshafati wa Yuda akarudi salama kwenye jumba lake la kifalme huko Yerusalemu. Yehu mwonaji, mwana wa Hanani, akapanda kwenda kuonana naye akamwambia Mfalme Yehoshafati, “Je, utawasaidia waovu na kuwapenda wale wanaomchukia BWANA? Kwa sababu ya jambo hili, ghadhabu ya BWANA iko juu yako.