2 Mambo ya Nyakati 15:1-2
2 Mambo ya Nyakati 15:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Roho ya Mungu ilimjia Azaria mwana wa Odedi, naye akatoka kwenda kumlaki mfalme Asa, akamwambia, “Nisikilize, ee mfalme Asa na watu wote wa Yuda na Benyamini! Mwenyezi-Mungu yu pamoja nanyi, ikiwa mtakuwa pamoja naye. Mkimtafuta, mtampata, lakini mkimwacha naye atawaacha.
2 Mambo ya Nyakati 15:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo Roho ya Mungu ikamjia Azaria mwana wa Odedi; naye akatoka ili amlaki Asa, akamwambia, Nisikieni, Ee Asa, na Yuda wote na Benyamini; BWANA yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi.

2 Mambo ya Nyakati 15:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo roho ya Mungu ikamjia Azaria mwana wa Odedi; naye akatoka ili amlaki Asa, akamwambia, Nisikieni, Ee Asa, na Yuda wote na Benyamini; BWANA yu pamoja nanyi, mkiwa pamoja naye; nanyi mkimtafuta ataonekana kwenu; lakini mkimwacha atawaacha ninyi.
2 Mambo ya Nyakati 15:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Roho wa Mungu akamjia Azaria mwana wa Odedi. Akatoka ili kumlaki Asa na kumwambia, “Nisikilizeni, Asa na Yuda wote na Benyamini. BWANA yu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye. Mkimtafuta, ataonekana kwenu, lakini mkimwacha, naye atawaacha.