2 Mambo ya Nyakati 11:1-4
2 Mambo ya Nyakati 11:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Rehoboamu alipofika Yerusalemu, alikusanya askari stadi180,000 wa makabila ya Yuda na Benyamini, apate kupigana na Israeli, ili ajirudishie huo ufalme. Lakini ujumbe wa Mungu ulimjia Shemaya mtu wa Mungu, kusema: “Mwambie Rehoboamu mwana wa Solomoni, mfalme wa Yuda na Waisraeli wote katika Yuda na Benyamini ya kwamba mimi Bwana nasema, ‘Msiende wala msipigane na ndugu zenu. Rudini kila mtu nyumbani kwake, maana hayo yaliyotokea ni kama nilivyopanga.’” Basi wakatii ujumbe wa Mwenyezi-Mungu, wakarudi nyumbani, wala hawakwenda kupigana na Yeroboamu.
2 Mambo ya Nyakati 11:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hata Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba ya Yuda na Benyamini, watu wateule elfu mia moja na themanini waliokuwa hodari, watu wa vita, ili wapigane juu ya Israeli, ili wamrudishie Rehoboamu huo ufalme. Lakini neno la BWANA likamjia Shemaya mtu wa Mungu, kusema, Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, uwaambie na Israeli wote waliomo Yuda na Benyamini, ukisema, BWANA asema hivi, Hamtapanda wala kupigana na ndugu zenu; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi wakayatii maneno ya BWANA wakarudi wasiende kupigana na Yeroboamu.
2 Mambo ya Nyakati 11:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hata Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba ya Yuda na Benyamini, watu wateule mia na themanini elfu waliokuwa hodari, watu wa vita, ili wapigane juu ya Israeli, ili wamrudishie Rehoboamu huo ufalme. Lakini neno la BWANA likamjia Shemaya mtu wa Mungu, kusema, Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, uwaambie na Israeli wote waliomo Yuda na Benyamini, ukisema, BWANA asema hivi, Hamtapanda wala kupigana na ndugu zenu; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakayasikiliza maneno ya BWANA, wakarudi katika kumwendea Yeroboamu.
2 Mambo ya Nyakati 11:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba ya Yuda na ya Benyamini, vijana wenye uwezo elfu mia moja na themanini, ili kufanya vita dhidi ya nyumba ya Israeli, na kuurudisha ufalme kwa Rehoboamu. Lakini neno hili la BWANA likamjia Shemaya mtu wa Mungu: “Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani mfalme wa Yuda, na Waisraeli wote walio Yuda na Benyamini, ‘Hili ndilo asemalo BWANA: Msipande kupigana dhidi ya ndugu zenu. Nendeni nyumbani, kila mmoja wenu, kwa kuwa hili nimelitenda mimi.’ ” Kwa hiyo wakalitii neno la BWANA na kurudi, wakaacha kwenda kupigana dhidi ya Yeroboamu.