2 Mambo ya Nyakati 10:18 - Compare All Versions
2 Mambo ya Nyakati 10:18 BHN (Biblia Habari Njema)
Kisha mfalme Rehoboamu alipomtuma Hadoramu aliyekuwa mnyapara mkuu wa kazi za kulazimishwa, watu wa Israeli walimpiga mawe, wakamuua. Ndipo Rehoboamu alipopanda gari lake haraka akakimbilia Yerusalemu.
2 Mambo ya Nyakati 10:18 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, msimamizi wa shokoa; nao wana wa Israeli wakamtupia mawe, hata akafa. Mfalme Rehoboamu akafanya haraka kupanda garini mwake, ili akimbilie Yerusalemu.
2 Mambo ya Nyakati 10:18 SRUV (Swahili Revised Union Version)
Ndipo mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, msimamizi wa shokoa; nao wana wa Israeli wakampiga kwa mawe hadi akafa. Mfalme Rehoboamu akafanya haraka kupanda garini mwake, ili akimbilie Yerusalemu.
2 Mambo ya Nyakati 10:18 NEN (Neno)
Mfalme Rehoboamu akamtuma Adoniramu aliyekuwa msimamizi wa wale waliofanya kazi ngumu kwa kulazimishwa, lakini Israeli wote wakampiga kwa mawe hadi akafa. Hata hivyo, Mfalme Rehoboamu akafanikiwa kuingia kwenye gari lake la vita, akatorokea Yerusalemu.