1 Timotheo 3:2-3
1 Timotheo 3:2-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, askofu anapaswa kuwa mtu asiye na lawama; anapaswa awe na mke mmoja tu, awe mwenye kiasi, nidhamu na utaratibu; ni lazima awe mkarimu na anayeweza kufundisha; asiwe mlevi au mtu wa matata, bali awe mpole, apendaye amani; asiwe mtu wa kupenda fedha
Shirikisha
Soma 1 Timotheo 31 Timotheo 3:2-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkarimu, ajuaye kufundisha; asiwe mtu wa kulewa, asiye dhalimu; bali awe mpole; asiwe mbishi, wala asiwe mwenye kupenda fedha
Shirikisha
Soma 1 Timotheo 31 Timotheo 3:2-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha
Shirikisha
Soma 1 Timotheo 3