1 Timotheo 1:13-14
1 Timotheo 1:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
ingawa pale awali mimi nilimtukana na kumtesa na kumdhulumu. Lakini Mungu alinionea huruma, kwa sababu sikuwa na imani bado, na hivyo sikujua nilichokuwa ninafanya. Lakini Bwana wetu alinijalia neema yake kwa wingi, akanipa imani na upendo katika kuungana na Kristo Yesu.
1 Timotheo 1:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
ingawa hapo awali nilikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye ujeuri, lakini nilipata rehema kwa kuwa nilifanya hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani. Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu.
1 Timotheo 1:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
ingawa hapo kwanza nalikuwa mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri, lakini nalipata rehema kwa kuwa nalitenda hivyo kwa ujinga, na kwa kutokuwa na imani. Na neema ya Bwana wetu ilizidi sana, pamoja na imani na pendo lililo katika Kristo Yesu.
1 Timotheo 1:13-14 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ingawa wakati fulani nilikuwa mwenye kukufuru, mtesaji na mwenye jeuri, lakini nilipata rehema kwa sababu nilitenda hivyo kwa kutojua na kutoamini kwangu. Neema ya Bwana wetu ilimiminwa juu yangu kwa wingi, ikiambatana na imani na upendo ulio katika Kristo Yesu.