1 Wathesalonike 5:3-5
1 Wathesalonike 5:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Watu watakapokuwa wanasema: “Kila kitu ni shwari na salama”, ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo. Lakini nyinyi, ndugu, hamko gizani, na siku hiyo haipaswi kuwajieni ghafla kama vile mwizi. Nyinyi nyote ni watu mnaoishi katika mwanga, watu wa mchana. Sisi si watu wa usiku, wala wa giza.
1 Wathesalonike 5:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. Bali ninyi, ndugu, hamko gizani, hata siku ile iwapate kama mwizi. Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
1 Wathesalonike 5:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa. Bali ninyi, ndugu, hammo gizani, hata siku ile iwapate kama mwivi. Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa nuru, na wana wa mchana; sisi si wa usiku, wala wa giza.
1 Wathesalonike 5:3-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula, kama vile uchungu unavyomjia mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka. Bali ninyi, ndugu, hampo gizani hata siku ile iwakute ghafula kama mwizi. Ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi si wana wa giza wala wa usiku.