1 Wathesalonike 5:2-3
1 Wathesalonike 5:2-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana nyinyi wenyewe mwajua kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi ajavyo usiku. Watu watakapokuwa wanasema: “Kila kitu ni shwari na salama”, ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo.
1 Wathesalonike 5:2-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana ninyi wenyewe mnajua hakika ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwizi ajavyo usiku. Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafla, kama vile uchungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
1 Wathesalonike 5:2-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku. Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula, kama vile utungu umjiavyo mwenye mimba, wala hakika hawataokolewa.
1 Wathesalonike 5:2-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
kwa kuwa mnajua vyema kwamba siku ya Bwana itakuja kama mwizi anavyokuja usiku. Watu wanaposema, “Kuna amani na salama,” maangamizi huwajia ghafula, kama vile uchungu unavyomjia mwanamke mwenye mimba; nao hakika hawatatoroka.