1 Wathesalonike 4:3-5
1 Wathesalonike 4:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu anataka nyinyi muwe watakatifu na mjiepushe kabisa na maisha ya zinaa. Kila mwanamume anapaswa kujua namna ya kuishi na mkewe kwa utakatifu na heshima, na si kwa tamaa mbaya kama watu wa mataifa mengine wasiomjua Mungu.
1 Wathesalonike 4:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.
1 Wathesalonike 4:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu.
1 Wathesalonike 4:3-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mapenzi ya Mungu ni ninyi mtakaswe, ili mjiepushe na uasherati, na kila mmoja wenu ajifunze kuutawala mwili wake mwenyewe katika utakatifu na heshima, bali si kwa tamaa mbaya kama watu wa Mataifa wasiomjua Mungu.