1 Wathesalonike 4:13-14
1 Wathesalonike 4:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Ndugu, twataka mjue ukweli kuhusu wale ambao wamekwisha fariki dunia, ili msipatwe na huzuni kama watu wengine wasio na matumaini. Sisi tunaamini kwamba Yesu alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.
1 Wathesalonike 4:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa tunaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
1 Wathesalonike 4:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.
1 Wathesalonike 4:13-14 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Lakini ndugu, hatutaki mkose kujua kuhusu wale waliolala katika mauti, ili msihuzunike kama watu wengine wasiokuwa na tumaini. Tunaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka. Na kwa hivyo, tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja naye wale waliolala katika Yesu.