1 Wathesalonike 4:1-2
1 Wathesalonike 4:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Hatimaye, ndugu zangu, mmejifunza kutoka kwetu namna mnavyopaswa kuishi ili kumpendeza Mungu. Na kweli mmekuwa mnaishi hivyo. Sasa tunawaombeni na kuwasihi kwa jina la Bwana Yesu mfanye vema zaidi. Maana mnayajua yale maagizo tuliyowapeni kwa mamlaka ya Bwana Yesu.
1 Wathesalonike 4:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Iliyobaki, ndugu, tunawasihi na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana. Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.
1 Wathesalonike 4:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Iliyobaki, ndugu, tunakusihini na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana. Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu.
1 Wathesalonike 4:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Na kuhusu mambo mengine, ndugu, tuliwafundisha jinsi ya kuishi ili kumpendeza Mungu, kama vile mnavyoishi. Sasa tunawaomba na kuwasihi katika Bwana Yesu mfanye hivi zaidi na zaidi. Kwa kuwa mnajua maagizo tuliyowapa kwa mamlaka ya Bwana Yesu.