1 Wathesalonike 3:4-5
1 Wathesalonike 3:4-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana, tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwaambieni kwamba tutateswa; na kama mjuavyo, ndivyo ilivyotukia. Ndio maana nilimtuma Timotheo kwenu. Sikuweza kungoja zaidi, na hivyo nilimtuma nipate habari za imani yenu. Isije ikawa labda Mshawishi aliwajaribuni na kazi yote tuliyofanya miongoni mwenu ikapotea bure!
1 Wathesalonike 3:4-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa kuwa tulipokuwapo kwenu tulitangulia kuwaambia kwamba tutapata dhiki, kama ilivyotukia, nanyi mnajua. Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nilituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida.
1 Wathesalonike 3:4-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa kuwa tulipokuwapo kwenu tulitangulia kuwaambia kwamba tutapata dhiki, kama ilivyotukia, nanyi mwajua. Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida.
1 Wathesalonike 3:4-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa kweli, tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaambia mara kwa mara kwamba tutateswa na imekuwa hivyo kama mnavyojua. Kwa sababu hii niliposhindwa kuvumilia zaidi, nilimtuma mtu ili nipate habari za imani yenu. Niliogopa kwamba kwa njia fulani yule mjaribu asiwe amewajaribu, nasi tukawa tumejitaabisha bure.