1 Wathesalonike 1:9-10
1 Wathesalonike 1:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Watu hao wanazungumza juu ya ziara yetu kwenu: Jinsi mlivyotukaribisha, jinsi mlivyoziacha sanamu, mkamgeukia Mungu aliye hai na wa kweli, na sasa mwamngojea Mwanae ashuke kutoka mbinguni, yaani Yesu, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu na ambaye anatuokoa katika ghadhabu ya Mungu inayokuja.
1 Wathesalonike 1:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli; na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa kutoka kwa ghadhabu itakayokuja.
1 Wathesalonike 1:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kwa kuwa wao wenyewe wanatangaza habari zetu, jinsi kulivyokuwa kuingia kwetu kwenu; na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaziacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai, wa kweli; na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa na ghadhabu itakayokuja.
1 Wathesalonike 1:9-10 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kwa maana watu wa maeneo hayo wenyewe wanaeleza jinsi mlivyotupokea na jinsi mlivyomgeukia Mungu mkaacha sanamu, ili kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli, na ili kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu: yaani Yesu, yeye aliyetuokoa kutoka ghadhabu inayokuja.