1 Wathesalonike 1:1-2
1 Wathesalonike 1:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Mimi Paulo, Silwano na Timotheo, kwa jumuiya ya kanisa la Thesalonike, ambayo ni watu wake Mungu Baba, na wa Bwana Yesu Kristo. Tunawatakieni neema na amani. Tunamshukuru Mungu daima kwa ajili yenu nyinyi nyote na kuwakumbukeni daima katika sala zetu.
1 Wathesalonike 1:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Paulo, Silwano na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba, na katika Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani. Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu.
1 Wathesalonike 1:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Paulo, na Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike, lililo katika Mungu Baba, na katika Bwana Yesu Kristo. Neema na iwe kwenu na amani. Twamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu nyote, tukiwataja katika maombi yetu.
1 Wathesalonike 1:1-2 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Paulo, Silvano na Timotheo. Kwa kanisa la Wathesalonike, ninyi mlio ndani ya Mungu Baba yetu na ndani ya Bwana Yesu Kristo. Neema iwe kwenu na amani. Siku zote tunamshukuru Mungu kwa ajili yenu ninyi nyote, tukiwataja kwenye maombi yetu daima.