1 Samueli 4:3
1 Samueli 4:3 Biblia Habari Njema (BHN)
Wanajeshi walionusurika walipowasili kambini, wazee wa Israeli walisema, “Kwa nini Mwenyezi-Mungu amewaacha Wafilisti watushinde leo? Twendeni tukalilete sanduku la agano la Mwenyezi-Mungu kutoka Shilo, ili aweze kwenda nasi vitani na kutuokoa kutoka na zetu.”
1 Samueli 4:3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hata watu walipofika kambini, wazee wa Israeli wakasema, Mbona BWANA ametupiga leo mbele ya Wafilisti? Twende tukalilete sanduku la Agano la BWANA kutoka Shilo hadi huku, lije kati yetu, na kutuokoa katika mikono ya adui zetu.
1 Samueli 4:3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hata watu walipofika kambini, wazee wa Israeli wakasema, Mbona BWANA ametupiga leo mbele ya Wafilisti? Twende tukalilete sanduku la agano la BWANA toka Shilo hata huku, lije kati yetu, na kutuokoa katika mikono ya adui zetu.
1 Samueli 4:3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Askari waliporudi kambini, wazee wa Israeli wakawauliza, “Kwa nini BWANA ameruhusu leo tushindwe mbele ya Wafilisti? Tuleteni Sanduku la Agano la BWANA kutoka Shilo, ili lipate kwenda pamoja nasi, na kutuokoa kutoka mikono ya adui zetu.”