1 Samueli 2:6-8
1 Samueli 2:6-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu huua na hufufua; yeye huwashusha chini kuzimu naye huwarudisha tena. Mwenyezi-Mungu huwafanya baadhi wawe maskini, na baadhi wawe matajiri. Wengine huwashusha, na wengine huwakweza. Huwainua maskini toka mavumbini; huwanyanyua wahitaji toka majivuni, akawaketisha pamoja na wakuu, na kuwarithisha viti vya heshima. Maana, minara ya dunia ni ya Mwenyezi-Mungu; yeye ameisimika dunia juu ya minara yake.
1 Samueli 2:6-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hadi kuzimu, tena huleta juu. BWANA hufukarisha mtu, na hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake.
1 Samueli 2:6-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA huua, naye hufanya kuwa hai; Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu. BWANA hufukarisha mtu, naye hutajirisha; Hushusha chini, tena huinua juu. Humwinua mnyonge kutoka mavumbini, Humpandisha mhitaji kutoka jaani, Ili awaketishe pamoja na wakuu, Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu; Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA, Naye ameuweka ulimwengu juu yake.
1 Samueli 2:6-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“BWANA huua na huhuisha; yeye hushusha hadi kaburini na hufufua. BWANA humfanya mtu maskini naye hutajirisha, hushusha na hukweza. Humwinua maskini kutoka mavumbini na humwinua mhitaji kutoka lundo la majivu; huwaketisha pamoja na wakuu, na kuwafanya warithi kiti cha utawala cha heshima.