1 Samueli 18:3-4
1 Samueli 18:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa kuwa Yonathani alimpenda Daudi kama roho yake, alifanya agano naye. Alivua vazi alilovaa na kumpa Daudi pamoja na silaha zake, hata upanga, upinde na mkanda wake.
1 Samueli 18:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe. Ndipo Yonathani akalivua joho alilokuwa amelivaa, akampa Daudi, na mavazi yake, hata na upanga wake pia, na upinde wake, na mshipi wake.
1 Samueli 18:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe. Ndipo Yonathani akalivua joho alilokuwa amelivaa, akampa Daudi, na mavazi yake, hata na upanga wake pia, na upinde wake, na mshipi wake.
1 Samueli 18:3-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Yonathani akafanya agano na Daudi kwa sababu alimpenda kama nafsi yake mwenyewe. Yonathani akavua joho alilokuwa amevaa na kumpa Daudi, pamoja na koti lake, silaha zake, hata pamoja na upanga wake, upinde wake na mshipi wake.