1 Samueli 12:14-18
1 Samueli 12:14-18 Biblia Habari Njema (BHN)
Kama mkimcha Mwenyezi-Mungu, na kumtumikia, na kusikiliza sauti yake bila kuiasi amri yake, kama nyinyi wenyewe pamoja na mfalme anayewatawala mkimfuata Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, basi mtafanikiwa. Lakini kama hamtasikiliza sauti ya Mwenyezi-Mungu, mkaasi amri yake, basi yeye atapambana nanyi pamoja na mfalme wenu. Kwa hiyo basi, tulieni na kulitazama jambo hilo kubwa ambalo Mwenyezi-Mungu atatenda mbele yenu. Je, sasa si wakati wa kuvuna ngano? Lakini mimi nitamwomba Mwenyezi-Mungu alete radi na mvua, nanyi mtatambua na kuona kuwa uovu wenu mliotenda mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa kujitakia mfalme, ni mkubwa.” Basi, Samueli akamwomba Mwenyezi-Mungu, naye akatuma radi na mvua katika siku hiyo. Watu wote wakamwogopa sana Mwenyezi-Mungu na Samueli.
1 Samueli 12:14-18 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kama mkimcha BWANA, na kumtumikia, na kuisikia sauti yake, msiiasi amri ya BWANA, tena kama ninyi, na mfalme anayewatawala, mkimfuata BWANA, Mungu wenu, vema! Bali msipoisikia sauti ya BWANA, mkiiasi amri ya BWANA, ndipo mkono wa BWANA utakuwa juu yenu, kama ulivyokuwa juu ya baba zenu. Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, BWANA atakalolitenda mbele ya macho yenu. Je! Leo si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, kwamba atume ngurumo na mvua; nanyi mtajua na kuona ya kuwa uovu wenu mlioufanya machoni pa BWANA, ni mwingi sana, kwa kujitakia mfalme. Basi Samweli akamwomba BWANA, naye BWANA akatuma ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa BWANA sana, na Samweli pia.
1 Samueli 12:14-18 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kama mkimcha BWANA, na kumtumikia, na kuisikia sauti yake, msiiasi amri ya BWANA, tena kama ninyi, na mfalme anayewatawala, mkimfuata BWANA, Mungu wenu, vema! Bali msipoisikia sauti ya BWANA, mkiiasi amri ya BWANA, ndipo mkono wa BWANA utakuwa juu yenu, kama ulivyokuwa juu ya baba zenu. Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, BWANA atakalolitenda mbele ya macho yenu. Leo je! Si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, kwamba apeleke ngurumo na mvua; nanyi mtajua na kuona ya kuwa uovu wenu ni mwingi sana, mlioufanya machoni pa BWANA, kwa kujitakia mfalme. Basi Samweli akamwomba BWANA, naye BWANA akapeleka ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa BWANA sana, na Samweli pia.
1 Samueli 12:14-18 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mkimcha BWANA, na kumtumikia na kumtii, nanyi msipoasi dhidi ya amri zake, ninyi pamoja na mfalme anayewatawala mkimfuata BWANA, Mungu wenu, mambo yatakuwa mema kwenu! Lakini kama hamkumtii BWANA, nanyi mkaasi dhidi ya amri zake, mkono wake utakuwa dhidi yenu, kama ulivyokuwa dhidi ya baba zenu. “Sasa basi, simameni kimya mkaone jambo hili kubwa ambalo BWANA anaenda kulifanya mbele ya macho yenu! Je, sasa si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA ili alete ngurumo na mvua. Nanyi mtatambua jambo hili lilivyo baya mlilolifanya mbele za macho ya BWANA mlipoomba mfalme.” Kisha Samweli akamwomba BWANA, na siku ile ile BWANA akatuma ngurumo na mvua. Hivyo watu wote wakamwogopa sana BWANA na Samweli.