1 Samueli 12:12-13
1 Samueli 12:12-13 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hata mlipomwona Nahashi, mfalme wa wana wa Amoni, amekuja kupigana nanyi, mliniambia, Sivyo, lakini mfalme atatutawala; ingawa BWANA, Mungu wenu, ni mfalme wenu. Basi sasa, mtazameni mfalme mliyemchagua na kumtaka; tazameni, BWANA ameweka mfalme juu yenu.
1 Samueli 12:12-13 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini mlipomwona mfalme Nahashi wa Waamoni amekuja kuwashambulia, mkamkataa Mwenyezi-Mungu ambaye ndiye Mfalme wenu, mkaniambia, ‘La! Mfalme ndiye atakayetutawala.’ Sasa, mfalme mliyejichagulia ndiye huyu hapa. Mlimwomba Mwenyezi-Mungu awape mfalme, naye amewapa.
1 Samueli 12:12-13 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hata mlipomwona Nahashi, mfalme wa wana wa Amoni, amekuja kupigana nanyi, mliniambia, Sivyo, lakini mfalme atatutawala; ingawa BWANA, Mungu wenu, ni mfalme wenu. Basi sasa, mtazameni mfalme mliyemchagua na kumtaka; tazameni, BWANA ameweka mfalme juu yenu.
1 Samueli 12:12-13 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Lakini mlipomwona yule Nahashi mfalme wa Waamoni anakuja dhidi yenu, mliniambia, ‘Hapana, tunataka mfalme atutawale,’ hata ingawa BWANA Mungu wenu alikuwa mfalme wenu. Sasa huyu hapa ndiye mfalme mliyemchagua, yule mliyeomba; tazameni, BWANA amemweka mfalme juu yenu.