1 Samueli 12:1-25
1 Samueli 12:1-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Samueli akawaambia Waisraeli wote, “Yote mliyoniambia, nimeyasikiliza. Nimemtawaza mfalme juu yenu. Sasa, mnaye mfalme wa kuwaongoza. Kwa upande wangu, mimi ni mzee mwenye mvi, na watoto wangu wa kiume wako pamoja nanyi. Nimekuwa kiongozi wenu tangu nilipokuwa kijana mpaka sasa. Niko hapa, na kama nimefanya tendo lolote lile baya, basi, toeni ushahidi mbele ya Mwenyezi-Mungu na mbele ya mfalme wake mteule. Je, nimepora fahali au punda wa mtu yeyote? Je, nimempunja mtu yeyote? Je, nimemkandamiza mtu yeyote? Je, nimepokea rushwa kwa mtu yeyote ili kupotosha haki? Nami nitamrudishia chochote kile.” Watu wakamjibu, “Kamwe hujatudanganya, hujatukandamiza, wala hujachukua kitu chochote kwa mtu.” Samueli akajibu, “Mwenyezi-Mungu ni shahidi juu yenu, na mfalme wake mteule leo ni shahidi kuwa mmeniona sina hatia.” Wao wakajibu: “Yeye ni shahidi.” Samueli akawaambia, “Mwenyezi-Mungu ndiye aliyemteua Mose na Aroni na kuwatoa babu zenu nchini Misri. Sasa simameni papo hapo mlipo ili mimi na nyinyi tuhukumiwe mbele ya Mwenyezi-Mungu, nami nitawahutubia kuhusu matendo yake ya ajabu ambayo aliyatenda ili kuwaokoa nyinyi na babu zenu. “Yakobo na jamaa yake walipokwenda Misri, na Wamisri walipowakandamiza, babu zenu walimlilia Mwenyezi-Mungu; naye akawatuma Mose na Aroni ambao waliwatoa babu zenu nchini Misri na kuwafanya mkae katika nchi hii. Lakini wao walimsahau Mwenyezi-Mungu, Mungu wao, naye akawatia mikononi mwa Sisera, kamanda wa jeshi la Hazori, na mikononi mwa Wafilisti na mikononi mwa mfalme wa Moabu. Mataifa hayo yalipigana na babu zenu na kuwashinda. Babu zenu wakamlilia Mwenyezi-Mungu, wakisema, ‘Tumefanya dhambi kwa sababu tumekuacha wewe Mwenyezi-Mungu, kwa kutumikia Mabaali na Maashtarothi. Tuokoe kutoka mikononi mwa adui zetu, nasi tutakutumikia’. Ndipo Mwenyezi-Mungu alipomtuma Yerubaali, na baadaye akamtuma Bedani, kisha Yeftha, na mwishowe akanituma mimi Samueli. Kila mmoja wetu aliwaokoa kutoka kwa adui zenu waliowazunguka, nanyi mkaishi kwa amani. Lakini mlipomwona mfalme Nahashi wa Waamoni amekuja kuwashambulia, mkamkataa Mwenyezi-Mungu ambaye ndiye Mfalme wenu, mkaniambia, ‘La! Mfalme ndiye atakayetutawala.’ Sasa, mfalme mliyejichagulia ndiye huyu hapa. Mlimwomba Mwenyezi-Mungu awape mfalme, naye amewapa. Kama mkimcha Mwenyezi-Mungu, na kumtumikia, na kusikiliza sauti yake bila kuiasi amri yake, kama nyinyi wenyewe pamoja na mfalme anayewatawala mkimfuata Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, basi mtafanikiwa. Lakini kama hamtasikiliza sauti ya Mwenyezi-Mungu, mkaasi amri yake, basi yeye atapambana nanyi pamoja na mfalme wenu. Kwa hiyo basi, tulieni na kulitazama jambo hilo kubwa ambalo Mwenyezi-Mungu atatenda mbele yenu. Je, sasa si wakati wa kuvuna ngano? Lakini mimi nitamwomba Mwenyezi-Mungu alete radi na mvua, nanyi mtatambua na kuona kuwa uovu wenu mliotenda mbele ya Mwenyezi-Mungu kwa kujitakia mfalme, ni mkubwa.” Basi, Samueli akamwomba Mwenyezi-Mungu, naye akatuma radi na mvua katika siku hiyo. Watu wote wakamwogopa sana Mwenyezi-Mungu na Samueli. Hivyo wakamwambia Samueli, “Tafadhali utuombee sisi watumishi wako kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ili tusife; kwa sababu tumezidisha dhambi zetu kwa uovu huo wa kujitakia mfalme.” Samueli akawajibu, “Msiogope; ingawa mmefanya uovu huu, msiache kumfuata Mwenyezi-Mungu, ila mtumikieni kwa moyo wenu wote. Msiifuate miungu ya uongo isiyo na faida wala haiwezi kuwaokoa, maana ni ya uongo. Kwa heshima ya jina lake kuu, Mwenyezi-Mungu hatawatupa watu wake kwa sababu amependa kuwafanya nyinyi muwe watu wake. Tena kwa upande wangu haitatokea niache kuwaombea kwa Mwenyezi-Mungu; kufanya hivyo itakuwa kumkosea Mwenyezi-Mungu. Nitaendelea kuwafundisha njia njema na ya haki. Basi, nyinyi mcheni Mwenyezi-Mungu na kumtumikia kwa uaminifu kwa moyo wenu wote. Kumbukeni yale mambo makuu aliyowatendea. Lakini kama mkiendelea kutenda maovu, mtaangamia nyinyi wenyewe pamoja na mfalme wenu.”
1 Samueli 12:1-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha Samweli akawaambia Israeli wote, Angalieni, nimeisikiliza sauti yenu katika hayo yote mliyoniambia, nami nimemtawaza mfalme juu yenu. Basi sasa, angalieni, mfalme anakwenda mbele yenu; na mimi ni mzee, mwenye mvi; tena, tazameni, wana wangu wapo pamoja nanyi; nami nimekwenda mbele yenu toka ujana wangu hata leo. Nami nipo hapa; basi, mnishuhudie mbele za BWANA, na mbele ya masihi wake, nilitwaa ng'ombe wa nani? Au nilitwaa punda wa nani? Au ni nani niliyemdhulumu? Ni nani niliyemwonea? Au kwa mkono wa nani nimepokea rushwa inipofushe macho? Nami nitawarudishia ninyi. Nao wakasema, Hukutudhulumu, wala hukutuonea, wala hukupokea kitu kwa mkono wa mtu awaye yote. Akawaambia, BWANA ni shahidi juu yenu, na masihi wake ni shahidi leo, ya kuwa hamkuona kitu mkononi mwangu. Nao wakasema, Yeye ni shahidi. Samweli akawaambia watu, Ni yeye BWANA aliyewaweka Musa na Haruni, yeye ndiye aliyewatoa baba zenu kutoka nchi ya Misri. Basi sasa simameni, ili niwahutubie mbele za BWANA, kwa kutaja matendo yote ya haki ya BWANA, aliyowatendea ninyi na baba zenu. Yakobo alipokuwa ameingia Misri, na baba zenu walipomlilia BWANA, ndipo BWANA akawapeleka Musa na Haruni, nao wakawatoa baba zenu kutoka Misri, wakawakalisha mahali hapa. Lakini wakamsahau BWANA, Mungu wao, naye akawauza na kuwatia katika mikono ya Sisera, jemadari wa jeshi la Hazori, na katika mikono ya Wafilisti, na katika mikono ya mfalme wa Moabu, nao wakapigana nao. Nao wakamlilia BWANA, wakasema, Tumefanya dhambi, kwa kuwa tumemwacha BWANA, na kuwatumikia Mabaali na Maashtorethi; lakini sasa tuokoe kutoka kwa mikono ya adui zetu, nasi tutakutumikia wewe. BWANA akawatuma Yerubaali, na Baraka, na Yeftha, na Samweli, akawaokoa ninyi kutoka kwa mikono ya adui zenu pande zote, nanyi mkakaa salama. Hata mlipomwona Nahashi, mfalme wa wana wa Amoni, amekuja kupigana nanyi, mliniambia, Sivyo, lakini mfalme atatutawala; ingawa BWANA, Mungu wenu, ni mfalme wenu. Basi sasa, mtazameni mfalme mliyemchagua na kumtaka; tazameni, BWANA ameweka mfalme juu yenu. Kama mkimcha BWANA, na kumtumikia, na kuisikia sauti yake, msiiasi amri ya BWANA, tena kama ninyi, na mfalme anayewatawala, mkimfuata BWANA, Mungu wenu, vema! Bali msipoisikia sauti ya BWANA, mkiiasi amri ya BWANA, ndipo mkono wa BWANA utakuwa juu yenu, kama ulivyokuwa juu ya baba zenu. Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, BWANA atakalolitenda mbele ya macho yenu. Je! Leo si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, kwamba atume ngurumo na mvua; nanyi mtajua na kuona ya kuwa uovu wenu mlioufanya machoni pa BWANA, ni mwingi sana, kwa kujitakia mfalme. Basi Samweli akamwomba BWANA, naye BWANA akatuma ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa BWANA sana, na Samweli pia. Watu wote wakamwambia Samweli, Tuombee watumishi wako kwa BWANA, Mungu wako, tusije tukafa; maana tumeongeza dhambi zetu zote kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme. Samweli akawaambia, Msiogope; ni kweli mmeutenda uovu huu wote; lakini msigeuke na kuacha kumfuata BWANA, bali mtumikieni BWANA kwa mioyo yenu yote. Wala msigeuke upande, maana, kufuata vitu vya ubatili, visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana BWANA hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza BWANA kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe. Lakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka Mcheni BWANA tu, mkamtumikie kwa kweli kwa mioyo yenu yote; maana, kumbukeni jinsi alivyowatendea mambo makuu. Lakini kama mkiendelea kutenda mabaya, mtaangamia, ninyi na mfalme wenu pia.
1 Samueli 12:1-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kisha Samweli akawaambia Israeli wote, Angalieni, nimeisikiliza sauti yenu katika hayo yote mliyoniambia, nami nimemtawaza mfalme juu yenu. Basi sasa, angalieni, mfalme anakwenda mbele yenu; na mimi ni mzee, mwenye mvi; tena, tazameni, wana wangu wapo pamoja nanyi; nami nimekwenda mbele yenu toka ujana wangu hata leo. Nami nipo hapa; basi, mnishuhudie mbele za BWANA, na mbele ya masihi wake, nalitwaa ng’ombe wa nani? Au nalitwaa punda wa nani? Au ni nani niliyemdhulumu? Ni nani niliyemwonea? Au kwa mkono wa nani nimepokea rushwa inipofushe macho? Nami nitawarudishia ninyi. Nao wakasema, hukutudhulumu, wala hukutuonea, wala hukupokea kitu kwa mkono wa mtu awaye yote. Akawaambia, BWANA ni shahidi juu yenu, na masihi wake ni shahidi leo, ya kuwa hamkuona kitu mkononi mwangu. Nao wakasema, Yeye ni shahidi. Samweli akawaambia watu, Ni yeye BWANA aliyewaweka Musa na Haruni, ndiye yeye aliyewatoa baba zenu kutoka nchi ya Misri. Basi sasa simameni, ili niwahutubie mbele za BWANA, kwa kutaja matendo yote ya haki ya BWANA, aliyowatendea ninyi na baba zenu. Yakobo alipokuwa ameingia Misri, na baba zenu walipomlilia BWANA, ndipo BWANA akawapeleka Musa na Haruni, nao wakawatoa baba zenu kutoka Misri, wakawakalisha mahali hapa. Lakini wakamsahau BWANA, Mungu wao, naye akawauza na kuwatia katika mikono ya Sisera, jemadari wa jeshi la Hazori, na katika mikono ya Wafilisti, na katika mikono ya mfalme wa Moabu, nao wakapigana nao. Nao wakamlilia BWANA, wakasema, Tumefanya dhambi, kwa kuwa tumemwacha BWANA, na kuwatumikia Mabaali na Maashtorethi; lakini sasa utuokoe na mikono ya adui zetu, nasi tutakutumikia wewe. BWANA akawatuma Yerubaali, na Baraka, na Yeftha, na Samweli, akawaokoa ninyi na mikono ya adui zenu pande zote, nanyi mkakaa salama. Hata mlipomwona Nahashi, mfalme wa wana wa Amoni, amekuja kupigana nanyi, mliniambia, Sivyo, lakini mfalme atatutawala; ingawa BWANA, Mungu wenu, ni mfalme wenu. Basi sasa, mtazameni mfalme mliyemchagua na kumtaka; tazameni, BWANA ameweka mfalme juu yenu. Kama mkimcha BWANA, na kumtumikia, na kuisikia sauti yake, msiiasi amri ya BWANA, tena kama ninyi, na mfalme anayewatawala, mkimfuata BWANA, Mungu wenu, vema! Bali msipoisikia sauti ya BWANA, mkiiasi amri ya BWANA, ndipo mkono wa BWANA utakuwa juu yenu, kama ulivyokuwa juu ya baba zenu. Na sasa simameni, mkalione jambo hili kubwa, BWANA atakalolitenda mbele ya macho yenu. Leo je! Si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA, kwamba apeleke ngurumo na mvua; nanyi mtajua na kuona ya kuwa uovu wenu ni mwingi sana, mlioufanya machoni pa BWANA, kwa kujitakia mfalme. Basi Samweli akamwomba BWANA, naye BWANA akapeleka ngurumo na mvua siku ile; nao watu wote wakamwogopa BWANA sana, na Samweli pia. Watu wote wakamwambia Samweli, Utuombee sisi watumwa wako kwa BWANA, Mungu wako, tusije tukafa; maana tumeongeza dhambi zetu zote kwa uovu huu, wa kujitakia mfalme. Samweli akawaambia, Msiogope; ni kweli mmeutenda uovu huu wote; lakini msigeuke na kuacha kumfuata BWANA, bali mtumikieni BWANA kwa mioyo yenu yote. Wala msigeuke upande, maana, kufuata vitu vya ubatili, visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana BWANA hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza BWANA kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe. Walakini mimi, hasha! Nisimtende BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi; lakini nitawaelimisha katika njia iliyo njema, na kunyoka Mcheni BWANA tu, mkamtumikie kwa kweli kwa mioyo yenu yote; maana, kumbukeni jinsi alivyowatendea mambo makuu. Lakini kama mkiendelea kutenda mabaya, mtaangamia, ninyi na mfalme wenu pia.
1 Samueli 12:1-25 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Samweli akawaambia Israeli wote, “Nimesikiliza kila kitu mlichoniambia nami nimewawekea mfalme juu yenu. Sasa mnaye mfalme kama kiongozi wenu. Lakini mimi ni mzee na nina mvi, nao wanangu wapo hapa pamoja nanyi. Nimekuwa kiongozi wenu tangu ujana wangu hadi siku hii ya leo. Mimi ninasimama hapa. Shuhudieni dhidi yangu mbele za BWANA na mpakwa mafuta wake. Nimechukua maksai wa nani? Nimechukua punda wa nani? Ni nani nimepata kumdanganya? Nimemdhulumu nani? Nimepokea rushwa kutoka kwa nani ili nifumbe macho yangu? Kama nimefanya chochote katika hivi, nitawarudishia.” Wakajibu, “Hujatudanganya wala kutudhulumu. Hujapokea chochote kutoka mkono wa mtu yeyote.” Samweli akawaambia, “BWANA ni shahidi dhidi yenu, pia mpakwa mafuta wake ni shahidi siku hii ya leo, kwamba hamkukuta chochote mkononi mwangu.” Wakasema, “Yeye ni shahidi.” Kisha Samweli akawaambia watu, “BWANA ndiye alimchagua Musa na Haruni, na kuwaleta baba zenu akiwapandisha kutoka Misri. Sasa basi, simameni hapa, kwa sababu nitakabiliana nanyi kwa ushahidi mbele za BWANA wa matendo yote ya haki yaliyofanywa na BWANA kwenu na kwa baba zenu. “Baada ya Yakobo kuingia Misri, walimlilia BWANA awasaidie, naye BWANA akawatuma Musa na Haruni, ambao waliwatoa baba zenu kutoka Misri na kuwakalisha mahali hapa. “Lakini wakamsahau BWANA Mungu wao, hivyo Mungu akawauza katika mkono wa Sisera, jemadari wa jeshi la Hazori na katika mikono ya Wafilisti na mfalme wa Moabu, ambaye alipigana dhidi yao. Wakamlilia BWANA na kusema, ‘Tumetenda dhambi; tumemwacha BWANA na kutumikia Mabaali na Maashtorethi. Lakini sasa tuokoe kutoka mikono ya adui zetu, nasi tutakutumikia.’ Ndipo BWANA akawatuma Yerub-Baali, Baraka, Yefta na Samweli, naye akawaokoa kutoka mikononi mwa adui zenu kila upande, ili ninyi mpate kukaa salama. “Lakini mlipomwona yule Nahashi mfalme wa Waamoni anakuja dhidi yenu, mliniambia, ‘Hapana, tunataka mfalme atutawale,’ hata ingawa BWANA Mungu wenu alikuwa mfalme wenu. Sasa huyu hapa ndiye mfalme mliyemchagua, yule mliyeomba; tazameni, BWANA amemweka mfalme juu yenu. Mkimcha BWANA, na kumtumikia na kumtii, nanyi msipoasi dhidi ya amri zake, ninyi pamoja na mfalme anayewatawala mkimfuata BWANA, Mungu wenu, mambo yatakuwa mema kwenu! Lakini kama hamkumtii BWANA, nanyi mkaasi dhidi ya amri zake, mkono wake utakuwa dhidi yenu, kama ulivyokuwa dhidi ya baba zenu. “Sasa basi, simameni kimya mkaone jambo hili kubwa ambalo BWANA anaenda kulifanya mbele ya macho yenu! Je, sasa si mavuno ya ngano? Nitamwomba BWANA ili alete ngurumo na mvua. Nanyi mtatambua jambo hili lilivyo baya mlilolifanya mbele za macho ya BWANA mlipoomba mfalme.” Kisha Samweli akamwomba BWANA, na siku ile ile BWANA akatuma ngurumo na mvua. Hivyo watu wote wakamwogopa sana BWANA na Samweli. Watu wote wakamwambia Samweli, “Mwombe BWANA Mungu wako kwa ajili ya watumishi wako, ili tusije tukafa, kwa kuwa tumeongeza uovu juu ya dhambi zetu nyingine kwa kuomba mfalme.” Samweli akajibu, “Msiogope, mmefanya uovu huu wote; hata hivyo msimwache BWANA, bali mtumikieni BWANA kwa moyo wote. Msigeukie sanamu batili. Haziwezi kuwatendea jema, wala haziwezi kuwaokoa kwa sababu hazina maana. Kwa ajili ya jina lake kuu BWANA hatawakataa watu wake, kwa sababu ilimpendeza BWANA kuwafanya watu wake mwenyewe. Lakini iwe mbali nami kutenda dhambi dhidi ya BWANA kwa kushindwa kuwaombea. Mimi nitawafundisha njia iliyo njema na nyoofu. Lakini hakikisheni mnamcha BWANA na kumtumikia kwa uaminifu kwa moyo wote; tafakarini mambo makubwa aliyoyatenda kwa ajili yenu. Hata hivyo mkiendelea kufanya uovu, ninyi na mfalme wenu mtafutiliwa mbali!”