1 Samueli 1:24-28
1 Samueli 1:24-28 Biblia Habari Njema (BHN)
Alipomwachisha kunyonya alimpeleka pamoja na fahali wa miaka mitatu, gunia la unga na kiriba cha divai. Hana alimwingiza mtoto kwenye nyumba ya Mwenyezi-Mungu huko Shilo, naye mtoto alikuwa mdogo tu. Walipokwisha kumchinja yule fahali, walimpeleka mtoto kwa kuhani Eli. Hana akamwambia, “Ee bwana wangu, kama iishivyo roho yako, bwana wangu, mimi ndimi yule mwanamke aliyekuwa anasimama mbele yako akimwomba Mwenyezi-Mungu. Nilimwomba anipe mtoto huyu, na yeye alinipa kile nilichomwomba. Kwa sababu hiyo, mimi ninampa Mwenyezi-Mungu mtoto huyu; wakati wote atakapokuwa hai, ametolewa kwa Mwenyezi-Mungu.” Halafu, wakamwabudu Mwenyezi-Mungu hapo.
1 Samueli 1:24-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naye alipomwachisha kunyonya, akamchukua pamoja naye, na ng'ombe watatu, na efa moja ya unga, na chupa ya divai, akamleta nyumbani kwa BWANA, huko Shilo; na yule mtoto alikuwa mtoto mdogo. Nao wakamchinja huyo ng'ombe, wakamleta mtoto kwa Eli. Akasema, Ee bwana wangu, kama iishivyo roho yako, bwana wangu, mimi ndimi yule mwanamke aliyesimama karibu nawe hapa, nikimwomba BWANA. Niliomba nipewe mtoto huyu; BWANA akanipa dua yangu niliyomwomba; kwa sababu hiyo mimi nami nimempa BWANA mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa BWANA. Naye akamwabudu BWANA huko.
1 Samueli 1:24-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naye alipokuwa amekwisha kumwachisha maziwa, akamchukua pamoja naye, na ng’ombe watatu, na efa moja ya unga, na chupa ya divai, akamleta nyumbani kwa BWANA, huko Shilo; na yule mtoto alikuwa mtoto mdogo. Nao wakamchinja huyo ng’ombe, wakamleta mtoto kwa Eli. Akasema, Ee bwana wangu, kama iishivyo roho yako, bwana wangu, mimi ndimi yule mwanamke aliyesimama karibu nawe hapa, nikimwomba BWANA. Naliomba nipewe mtoto huyu; BWANA akanipa dua yangu niliyomwomba; kwa sababu hiyo mimi nami nimempa BWANA mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa BWANA. Naye akamwabudu BWANA huko.
1 Samueli 1:24-28 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baada ya mtoto kuachishwa kunyonya, Hana akamchukua huyo mtoto, akiwa mdogo hivyo hivyo, pamoja na fahali wa miaka mitatu, efa ya unga na kiriba cha divai, naye akamleta mtoto kwenye nyumba ya BWANA huko Shilo. Walipokwisha kumchinja yule fahali, wakamleta mtoto kwa Eli, naye Hana akamwambia Eli, “Hakika kama uishivyo, bwana wangu, mimi ndiye yule mama ambaye alisimama hapa karibu nawe akiomba kwa BWANA. Niliomba mtoto huyu, naye BWANA amenijalia kile nilichomwomba. Hivyo sasa ninamtoa kwa BWANA. Kwa maana maisha yake yote atakuwa ametolewa kwa BWANA.” Naye akamwabudu BWANA huko.