1 Wafalme 22:51-53
1 Wafalme 22:51-53 Biblia Habari Njema (BHN)
Mnamo mwaka wa kumi na saba wa utawala wa Yehoshafati, mfalme wa Yuda, Ahazia, mwana wa Ahabu, alianza kutawala Israeli. Alitawala kwa muda wa miaka miwili, kutoka Samaria. Ahazia alitenda maovu mbele ya Mwenyezi-Mungu; aliuiga mwenendo wa baba yake na mwenendo wa Yezebeli, mama yake, na wa Yeroboamu, mwana wa Nebati ambaye aliwafanya watu wa Israeli watende dhambi. Alimtumikia na kumwabudu Baali, akamkasirisha Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kwa kila jambo kama alivyofanya baba yake.
1 Wafalme 22:51-53 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ahazia mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli huko Samaria, katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akatawala miaka miwili juu ya Israeli. Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akaiendea njia ya babaye, na njia ya mamaye, na njia ya Yeroboamu mwana wa Nebati, aliyewakosesha Israeli. Akamtumikia Baali, akamwabudu, akamghadhibisha BWANA, Mungu wa Israeli, kwa mfano wa mambo yote aliyoyafanya baba yake.
1 Wafalme 22:51-53 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ahazia mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli huko Samaria, katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akatawala miaka miwili juu ya Israeli. Akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, akaiendea njia ya babaye, na njia ya mamaye, na njia ya Yeroboamu mwana wa Nebati, aliyewakosesha Israeli. Akamtumikia Baali, akamwabudu, akamghadhibisha BWANA, Mungu wa Israeli, kwa mfano wa mambo yote aliyoyafanya baba yake.
1 Wafalme 22:51-53 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ahazia mwana wa Ahabu akawa mfalme wa Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na saba wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. Naye akatawala katika Israeli kwa miaka miwili. Akafanya maovu machoni pa BWANA kwa sababu alienenda katika njia za baba yake na mama yake na katika njia za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli itende dhambi. Alimtumikia na kumwabudu Baali na kumghadhibisha BWANA, Mungu wa Israeli, kama vile baba yake alivyokuwa amefanya.