1 Wafalme 2:2-4
1 Wafalme 2:2-4 Biblia Habari Njema (BHN)
“Mwanangu, kama ilivyo kawaida kwa viumbe vyote kufa, siku zangu zimekwisha. Uwe imara na hodari. Timiza maagizo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ufuate njia zake na kushika masharti yake, amri zake, hukumu zake na kuheshimu maamuzi yake kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, ili upate kufanikiwa katika kila ufanyalo na kokote uendako, pia ili Mwenyezi-Mungu atimize ahadi yake aliyotoa aliponiambia kuwa, ikiwa wazawa wangu watatii amri zake na kumtumikia kwa uaminifu na kwa moyo wote, hakutakosekana mmoja wao kutawala Israeli nyakati zote.
1 Wafalme 2:2-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujioneshe kuwa shujaa na hodari; uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako; ili BWANA afanye imara neno lake alilonena kuhusu habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli.
1 Wafalme 2:2-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujionyeshe kuwa mwanamume; uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako; ili BWANA afanye imara neno lake alilonena kwa habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli.
1 Wafalme 2:2-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Akasema, “Ninakaribia kwenda njia ya dunia yote. Hivyo uwe hodari, jioneshe kuwa mwanaume, shika lile BWANA Mungu wako analokuagiza: Nenda katika njia zake, ushike maagizo na amri zake, sheria zake na kanuni zake, kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Musa, ili upate kustawi katika yote ufanyayo na popote utakapoenda, na ili BWANA aweze kunitimizia ahadi yake: ‘Kama wazao wako wakiangalia sana wanavyoishi, na wakienenda kwa uaminifu mbele zangu kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote, kamwe hutakosa kuwa na mtu kwenye kiti cha ufalme cha Israeli.’