1 Wafalme 2:1-3
1 Wafalme 2:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Daudi alipokaribia kufariki, alimwita mwanawe Solomoni, akampa wosia akisema, “Mwanangu, kama ilivyo kawaida kwa viumbe vyote kufa, siku zangu zimekwisha. Uwe imara na hodari. Timiza maagizo ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, ufuate njia zake na kushika masharti yake, amri zake, hukumu zake na kuheshimu maamuzi yake kama ilivyoandikwa katika sheria ya Mose, ili upate kufanikiwa katika kila ufanyalo na kokote uendako, pia
1 Wafalme 2:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi siku ya kufa kwake Daudi ikakaribia, akamwusia Sulemani mwanawe, akasema, Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujioneshe kuwa shujaa na hodari; uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako
1 Wafalme 2:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi siku ya kufa kwake Daudi ikakaribia, akamwusia Sulemani mwanawe, akasema, Mimi naenda njia ya ulimwengu wote; basi uwe hodari, ujionyeshe kuwa mwanamume; uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako
1 Wafalme 2:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Siku zilipokaribia za Daudi kufa, akampa mwanawe Sulemani agizo. Akasema, “Ninakaribia kwenda njia ya dunia yote. Hivyo uwe hodari, jioneshe kuwa mwanaume, shika lile BWANA Mungu wako analokuagiza: Nenda katika njia zake, ushike maagizo na amri zake, sheria zake na kanuni zake, kama ilivyoandikwa katika Sheria ya Musa, ili upate kustawi katika yote ufanyayo na popote utakapoenda