1 Wafalme 19:1-3
1 Wafalme 19:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Mfalme Ahabu alimsimulia mkewe Yezebeli mambo yote aliyofanya Elia na jinsi alivyowaua manabii wa Baali kwa upanga. Yezebeli akatuma mjumbe kwa Elia amwambie: “Miungu waniulie mbali, nakuapia, ikiwa saa hizi kesho sitakuwa nimekufanya kama mmoja wa hao manabii.” Elia akakimbilia mjini Beer-sheba mkoani Yuda, alikomwacha mtumishi wake
1 Wafalme 19:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi, Ahabu akamwambia Yezebeli habari ya mambo yote aliyoyafanya Eliya, na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga. Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao. Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko.
1 Wafalme 19:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi, Ahabu akamwambia Yezebeli habari ya mambo yote aliyoyafanya Eliya, na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga. Ndipo Yezebeli akampelekea Eliya mjumbe, kusema, Miungu wanifanyie hivyo na kuzidi, nisipokufanya roho yako kesho, panapo wakati huu, kama roho ya mmojawapo wa hao. Naye alipoona hayo, aliondoka, akaenda aihifadhi roho yake, akafika Beer-sheba, mji wa Yuda, akamwacha mtumishi wake huko.
1 Wafalme 19:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ahabu akamwambia Yezebeli kila kitu Eliya alichokuwa amefanya na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga. Hivyo Yezebeli akamtuma mjumbe kwa Eliya, kusema, “Miungu waniadhibu vikali zaidi, ikiwa kesho wakati kama huu sitakuwa nimeondoa uhai wako kama mmoja wa hao manabii.” Eliya aliogopa, na akatoroka kuokoa maisha yake. Alipofika Beer-Sheba katika Yuda, akamwacha mtumishi wake huko