1 Wafalme 18:1-4
1 Wafalme 18:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Ikawa baada ya siku nyingi, mnamo mwaka wa tatu wa ukame, neno hili la Mwenyezi-Mungu likamjia Elia: “Nenda ukajioneshe kwa mfalme Ahabu, halafu nitanyesha mvua nchini.” Basi, Elia akaenda kujionesha kwa Ahabu. Wakati huo, njaa ilikuwa kali sana huko Samaria. Basi, Ahabu akamwita Obadia msimamizi wa ikulu. (Obadia alikuwa mtu amchaye Mwenyezi-Mungu sana, na wakati Yezebeli alipowaua manabii wa Mwenyezi-Mungu, Obadia aliwachukua manabii 100, akawaficha hamsinihamsini pangoni, akawa anawapelekea chakula na maji).
1 Wafalme 18:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikawa baada ya siku nyingi, neno la BWANA likamjia Eliya, katika mwaka wa tatu, kusema, Nenda, ukajioneshe kwa Ahabu; nami nitaleta mvua juu ya nchi. Basi Eliya akaenda ili ajioneshe kwa Ahabu. Na njaa ilikuwa nzito katika Samaria. Ahabu akamwita Obadia, aliyekuwa juu ya nyumba yake; (na huyu Obadia alikuwa mwenye kumcha BWANA sana; kwa kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, Obadia akatwaa manabii mia moja, akawaficha hamsini hamsini katika pango, akawalisha chakula na kuwapa maji).
1 Wafalme 18:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa baada ya siku nyingi, neno la BWANA likamjia Eliya, katika mwaka wa tatu, kusema, Enenda, ukajionyeshe kwa Ahabu; nami nitaleta mvua juu ya nchi. Basi Eliya akaenda ili ajionyeshe kwa Ahabu. Na njaa ilikuwa nzito katika Samaria. Ahabu akamwita Obadia, aliyekuwa juu ya nyumba yake; (na huyu Obadia alikuwa mwenye kumcha BWANA sana; kwa kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, Obadia akatwaa manabii mia, akawaficha hamsini hamsini katika pango, akawalisha chakula na kuwapa maji).
1 Wafalme 18:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baada ya muda mrefu, katika mwaka wa tatu, neno la BWANA likamjia Eliya kusema, “Nenda ukajioneshe kwa Ahabu nami nitaleta mvua juu ya nchi.” Kwa hiyo Eliya akaenda kujionesha kwa Ahabu. Wakati huo njaa ilikuwa kali sana katika Samaria, naye Ahabu alikuwa amemwita Obadia aliyekuwa msimamizi wa jumba la mfalme. (Obadia alimcha BWANA sana. Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa BWANA, Obadia alikuwa amewachukua manabii mia moja na kuwaficha katika mapango mawili, hamsini kwenye kila moja, na akawa akiwapa chakula na maji.)