1 Wafalme 17:2-6
1 Wafalme 17:2-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha, neno la Mwenyezi-Mungu lilimjia Elia: “Ondoka hapa uelekee mashariki, ukajifiche penye kijito cha Kerithi kilichoko mashariki ya mto Yordani. Huko, utapata maji ya kunywa katika kijito hicho tena nimewaamuru kunguru wakuletee chakula.” Basi, Elia akatii agizo la Mwenyezi-Mungu, akaenda kukaa kwenye kijito cha Kerithi kilichoko mashariki ya mto Yordani. Kunguru wakawa wanamletea mkate na nyama, asubuhi na jioni; akapata na maji ya kunywa katika kijito hicho.
1 Wafalme 17:2-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Neno la BWANA likamjia, kusema, Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani. Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko. Basi akaenda akafanya kama alivyosema BWANA; kwa kuwa alikwenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani. Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito.
1 Wafalme 17:2-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Neno la BWANA likamjia, kusema, Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani. Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko. Basi akaenda akafanya kama alivyosema BWANA; kwa kuwa akaenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani. Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito.
1 Wafalme 17:2-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kisha neno la BWANA likamjia Eliya, kusema, “Ondoka hapa, elekea upande wa mashariki ukajifiche karibu na Kijito cha Kerithi, mashariki mwa Yordani. Utakunywa maji kutoka kile kijito, nami nimeagiza kunguru wakulishe huko.” Naye akafanya kama alivyoambiwa na BWANA. Akaenda katika Kijito cha Kerithi, mashariki mwa Yordani na akakaa huko. Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, naye akanywa maji kutoka kile kijito.