Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Yohane 5:7-9 - Compare All Versions

1 Yohane 5:7-9 BHN (Biblia Habari Njema)

Basi, wako mashahidi watatu: Roho, maji na damu; na ushahidi wa hawa watatu waafikiana. Ikiwa twaukubali ushahidi wa binadamu, ushahidi wa Mungu una uzito zaidi; na huu ndio ushahidi alioutoa Mungu mwenyewe juu ya Mwanae.

Shirikisha
1 Yohane 5 BHN

1 Yohane 5:7-9 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.

Shirikisha
1 Yohane 5 SRUV

1 Yohane 5:7-9 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Naye Roho ndiye ashuhudiaye, kwa sababu Roho ndiye kweli. Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. Kisha wako watatu washuhudiao duniani], Roho, na maji, na damu; na watatu hawa hupatana kwa habari moja. Tukiupokea ushuhuda wa wanadamu, ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi; kwa maana ushuhuda wa Mungu ndio huu, kwamba amemshuhudia Mwanawe.

Shirikisha
1 Yohane 5 SUV

1 Yohane 5:7-9 NEN (Neno)

Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni: hao ni Baba, Neno na Roho Mtakatifu. Hawa watatu ni umoja. Pia wako mashahidi watatu duniani]: hao ni Roho, Maji na Damu; hawa watatu wanakubaliana katika umoja. Kama tunaukubali ushuhuda wa wanadamu, basi ushuhuda wa Mungu ni mkuu zaidi, kwa kuwa huu ndio ushuhuda wa Mungu kwamba amemshuhudia Mwanawe.

Shirikisha
1 Yohane 5 NEN