1 Wakorintho 3:7-8
1 Wakorintho 3:7-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Wa maana si yule aliyepanda mbegu, au yule aliyemwagilia maji; wa maana ni Mungu aliyeiwezesha mbegu kuota. Yule aliyepanda na yule aliyemwagilia maji wote ni sawa, ingawa kila mmoja atapokea tuzo lake kufuatana na jitihada yake mwenyewe.
Shirikisha
Soma 1 Wakorintho 31 Wakorintho 3:7-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe kulingana na taabu yake mwenyewe.
Shirikisha
Soma 1 Wakorintho 3