1 Wakorintho 2:7-8
1 Wakorintho 2:7-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Hekima tunayotumia ni hekima ya siri ya Mungu, hekima iliyofichika, ambayo Mungu aliiazimia tangu mwanzo kwa ajili ya utukufu wetu. Ni hekima ambayo watawala wa dunia hii hawakuielewa; maana wangaliielewa, hawangalimsulubisha Bwana wa utukufu.
1 Wakorintho 2:7-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulubisha Bwana wa utukufu.
1 Wakorintho 2:7-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
bali twanena hekima ya Mungu katika siri, ile hekima iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu milele, kwa utukufu wetu; ambayo wenye kuitawala dunia hii hawaijui hata mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu
1 Wakorintho 2:7-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Sisi tunanena hekima ya Mungu ambayo ni siri, tena iliyofichika, ambayo Mungu aliikusudia kabla ya ulimwengu kuumbwa, kwa ajili ya utukufu wetu. Hakuna hata mtawala mmoja wa nyakati hizi aliyeelewa jambo hili. Kwa maana kama wangeelewa, hawangemsulubisha Bwana wa utukufu.