1 Wakorintho 2:1-5
1 Wakorintho 2:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Ndugu, mimi nilipokuja kwenu sikuwahubiria siri ya ujumbe wa Mungu kwa ufasaha wa lugha, au kwa hekima ya binadamu. Nilipokuwa kwenu niliamua kutojua chochote kile isipokuwa tu kumjua Yesu Kristo; naam, Kristo aliyesulubiwa. Nilipokuwa kwenu nilikuwa dhaifu, natetemeka kwa hofu nyingi. Hotuba zangu na mahubiri yangu sikuyatoa kwa maneno ya kuvutia na ya hekima, bali kwa uthibitisho mwingi na nguvu ya Roho. Nilifanya hivyo kusudi imani yenu ipate kutegemea nguvu ya Mungu, na si hekima ya binadamu.

1 Wakorintho 2:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubirie siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima. Maana niliazimu nisijue neno lolote kwenu ila Yesu Kristo, na yeye aliyesulubiwa. Nami nilikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na kwa kutetemeka sana. Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.
1 Wakorintho 2:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi, ndugu zangu, mimi nilipokuja kwenu, sikuja niwahubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima. Maana naliazimu nisijue neno lo lote kwenu ila Yesu Kristo, naye amesulibiwa. Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na hofu na matetemeko mengi. Na neno langu na kuhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho na za nguvu, ili imani yenu isiwe katika hekima ya wanadamu, bali katika nguvu za Mungu.
1 Wakorintho 2:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ndugu zangu nilipokuja kwenu, sikuja na maneno ya ushawishi wala hekima ya hali ya juu nilipowahubiria siri ya Mungu. Kwa kuwa niliamua kutokujua kitu chochote nilipokuwa nanyi, isipokuwa Yesu Kristo aliyesulubiwa. Mimi nilikuja kwenu nikiwa dhaifu na mwenye hofu na kwa kutetemeka sana. Kuhubiri kwangu na ujumbe wangu haukuwa kwa hekima na maneno ya ushawishi, bali kwa madhihirisho ya nguvu za Roho, ili imani yenu isiwe imejengwa katika hekima ya wanadamu bali katika nguvu za Mungu.