1 Wakorintho 14:27-28
1 Wakorintho 14:27-28 Biblia Habari Njema (BHN)
Wakiwapo watu wenye vipaji vya kusema kwa lugha ngeni, waseme wawili au watatu, si zaidi, tena mmojammoja; na aweko mtu wa kufafanua yanayosemwa. Lakini kama hakuna awezaye kufafanua, basi, mwenye kusema lugha ngeni anyamaze mkutanoni, aseme na nafsi yake mwenyewe na Mungu.
1 Wakorintho 14:27-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri. Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.
1 Wakorintho 14:27-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kama mtu akinena kwa lugha, wanene wawili au watatu, si zaidi, tena zamu kwa zamu, na mmoja na afasiri. Lakini asipokuwapo mwenye kufasiri na anyamaze katika kanisa; aseme na nafsi yake tena na Mungu.
1 Wakorintho 14:27-28 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kama mtu yeyote akinena kwa lugha, basi waseme watu wawili au watatu, si zaidi, mmoja baada ya mwingine, na lazima awepo mtu wa kutafsiri. Lakini kama hakuna mtu wa kutafsiri, hao watu na wanyamaze kimya kanisani na wanene na nafsi zao wenyewe na Mungu.