1 Mambo ya Nyakati 7:6-12
1 Mambo ya Nyakati 7:6-12 Biblia Habari Njema (BHN)
Benyamini alikuwa na wana watatu: Bela, Bekeri na Yediaeli. Bela alikuwa na wana watano: Esboni, Uzi, Uzieli, Yeremothi na Iri. Hawa walikuwa viongozi wa jamaa zao, na wanajeshi mashujaa. Walioandikishwa kwa kufuata koo, idadi ya wazawa wao ilikuwa 22,034. Bekeri alikuwa na wana tisa: Zemira, Yoashi, Eliezeri, Eliehonai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Wote hawa ni wazawa wa Bekeri. Waliandikishwa kwa koo kulingana na vizazi vyao kama viongozi wa jamaa zao, na idadi ya wazawa wao ilikuwa 20,200, wote wakiwa mashujaa wa vita. Yediaeli alikuwa na mwana mmoja, jina lake Bilhani. Bilhani alikuwa na wana: Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari. Wote hawa walikuwa wakuu wa jamaa katika koo zao na askari mashujaa wa vita. Kutokana na wazawa wao, kulipatikana wanaume 178,200, wanajeshi hodari tayari kabisa kwa vita. Shupimu na Hupimu pia walikuwa wa kabila hili. Dani alikuwa na mwana mmoja, jina lake Hushimu.
1 Mambo ya Nyakati 7:6-12 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wana wa Benyamini; Bela, na Bekeri, na Yediaeli, watatu. Na wana wa Bela; Esboni, na Uzi, na Uzieli, na Yerimothi, na Iri, watano; wakuu wa koo za baba zao, watu hodari wa vita; nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao watu elfu ishirini na mbili na thelathini na wanne. Na wana wa Bekeri; Zemira, na Yoashi, na Eliezeri, na Elioenai, na Omri, na Yeremothi, na Abiya, na Anathothi, na Alemethi. Hao wote ndio wana wa Bekeri. Nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao, katika vizazi vyao, wakuu wa koo za baba zao, watu hodari wa vita, jumla yao watu elfu ishirini na mia mbili. Na wana wa Yediaeli; Bilhani; na wana wa Bilhani; Yeushi, na Benyamini, na Ehudi, na Kenaana, na Zethani, na Tarshishi, na Ahishahari. Hao wote ndio wana wa Yediaeli, kulingana na wakuu wa koo za baba zao, watu hodari wa vita, elfu kumi na saba na mia mbili, wawezao kwenda vitani katika jeshi. Tena Shupimu, na Hupimu, wana wa Iri; na Hushimu, wana wa Aheri.
1 Mambo ya Nyakati 7:6-12 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wana wa Benyamini; Bela, na Bekeri, na Yediaeli, watatu. Na wana wa Bela; Esboni, na Uzi, na Uzieli, na Yerimothi, na Iri, watano; wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita; nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao watu ishirini na mbili elfu na thelathini na wanne. Na wana wa Bekeri; Zemira, na Yoashi, na Eliezeri, na Elioenai, na Omri, na Yeremothi, na Abiya, na Anathothi, na Alemethi. Hao wote ndio wana wa Bekeri. Nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao, katika vizazi vyao, wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita, jumla yao watu ishirini elfu na mia mbili. Na wana wa Yediaeli; Bilhani; na wana wa Bilhani; Yeushi, na Benyamini, na Ehudi, na Kenaana, na Zethani, na Tarshishi, na Ahishahari. Hao wote ndio wana wa Yediaeli, sawasawa na wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita, kumi na saba elfu na mia mbili, wawezao kwenda vitani katika jeshi. Tena Shupimu, na Hupimu, wana wa Iri; na Hushimu, wana wa Aheri.
1 Mambo ya Nyakati 7:6-12 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wana watatu wa Benyamini walikuwa: Bela, Bekeri na Yediaeli. Wana wa Bela walikuwa: Esboni, Uzi, Uzieli, Yerimothi na Iri; walikuwa viongozi wa jamaa zao; wote ni watano. Wapiganaji walioorodheshwa katika ukoo wao walikuwa elfu ishirini na mbili na thelathini na wanne (22,034). Wana wa Bekeri walikuwa: Zemira, Yoashi, Eliezeri, Elioenai, Omri, Yeremothi, Abiya, Anathothi na Alemethi. Hawa wote walikuwa wana wa Bekeri. Orodha ya ukoo wao iliyoandikwa viongozi wa jamaa zao walikuwa wapiganaji elfu ishirini na mia mbili. Mwana wa Yediaeli alikuwa: Bilhani. Wana wa Bilhani walikuwa: Yeushi, Benyamini, Ehudi, Kenaana, Zethani, Tarshishi na Ahishahari. Hawa wana wote wa Yediaeli walikuwa viongozi wa jamaa zao. Kulikuwa na wapiganaji elfu kumi na saba na mia mbili waliokuwa tayari kwa vita. Washupimu na Wahupimu walikuwa wazao wa Iri. Wahushimu walikuwa wazao wa Aheri.