1 Mambo ya Nyakati 7:13-40
1 Mambo ya Nyakati 7:13-40 Biblia Habari Njema (BHN)
Naftali alikuwa na wana wanne: Yaasieli, Guni, Yereri na Shalumu. Hao walikuwa wazawa wa Bilha. Manase alikuwa na wana wawili kutokana na suria wake Mwaramu: Asrieli na Makiri. Makiri alikuwa baba yake Gileadi. Makiri aliwazaa Hupimu na Shupimu. Jina la dada yake lilikuwa Maaka. Mwana wa pili wa Makiri alikuwa Selofehadi. Selofehadi alikuwa na mabinti peke yake. Maaka mkewe Makiri, alizaa mwana jina lake Pereshi. Jina la nduguye Pereshi lilikuwa Shereshi. Wanawe Shereshi walikuwa Ulamu na Rakemu. Rakemu alimzaa Bedani. Hawa wote ni wazawa wa Gileadi, mwana wa Makiri, mjukuu wa Manase. Hamo-lekethi, dada yake Gileadi, aliwazaa Ishhodi, Abiezeri na Mala. Wana wa Shemida walikuwa Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu. Hawa ndio wazawa wa Efraimu kutoka kizazi hadi kizazi: Shuthela, Beredi, Tahathi, Eleada, Tahathi, Zabadi na Shuthela. Mbali na Shuthela, Efraimu alikuwa na wana wengine wawili, Ezeri, na Eleadi, ambao waliuawa na wenyeji wa asili wa nchi ya Gathi kwa sababu walikwenda huko kuwanyanganya mifugo yao. Efraimu baba yao aliomboleza vifo vyao kwa siku nyingi sana, na ndugu zake wakaja kumfariji. Ndipo Efraimu akalala na mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana. Efraimu akampa jina Beria, kwa sababu ya maafa yaliyoipata jamaa yake. Efraimu alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliyeijenga miji ya Beth-horoni ya juu na chini, na Uzen-sheera. Efraimu alimzaa pia Refa ambaye alimzaa Reshefu, Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani, Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi, Amihudi akamzaa Elishama, Elishama akamzaa Nuni, Nuni akamzaa Yoshua. Milki zao na makao yao yalikuwa: Betheli na vitongoji vyake, Naraani uliokuwa upande wa mashariki, Gezeri uliokuwa upande wa magharibi pamoja na vitongoji vyake, Shekemu na vitongoji vyake, na Aya na vitongoji vyake. Na pia mipakani mwa wana wa Manase: Beth-sheani na vitongoji vyake, Taanaki na vitongoji vyake, Megido na vitongoji vyake na Dori na vitongoji vyake. Hiyo ndiyo miji walimoishi wazawa wa Yosefu, mwana wa Israeli. Hawa ndio wazawa wa Asheri. Asheri alikuwa na wana wanne: Imna, Ishva, Ishri na Beria, na binti mmoja jina lake Sera. Beria alikuwa na wana wawili: Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi. Heberi alikuwa na wana watatu: Yafleti, Shomeri na Hothamu, na binti mmoja jina lake Shua. Yafleti pia alikuwa na wana watatu: Pasaki, Bimhali na Ashvathi. Shemeri, nduguye, alikuwa na wana watatu: Roga, Yehuba na Aramu. Na Helemu, ndugu yake mwingine, alikuwa na wana wanne: Sofa, Imna, Sheleshi na Amali. Wana wa Sofa walikuwa Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra, Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani na Beera. Wana wa Yetheri walikuwa Yefune, Pispa na Ara. Wana wa Ula walikuwa Ara, Hanieli na Risia. Hao wote walikuwa wazawa wa Asheri na walikuwa wakuu wa jamaa zao, watu wateule na hodari wa vita. Idadi ya wale walioandikishwa kwa kufuata koo katika jeshi ilikuwa 26,000.
1 Mambo ya Nyakati 7:13-40 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yeseri, na Shalumu; wana wa Bilha. Wana wa Manase; Asrieli, ambaye suria yake, Mwarami, alimzalia, akamzalia na Makiri babaye Gileadi; naye Makiri akatwaa mke kwa Hupimu na Shupimu, ambao dada yao aliitwa Maaka; na wa pili akaitwa jina lake Selofehadi; na Selofehadi alikuwa na binti. Na Maaka mkewe Makiri, akamzalia mwana, akamwita jina lake Pereshi; na jina la nduguye aliitwa Shereshi; na wanawe walikuwa Ulamu, na Rakemu. Na wana wa Ulamu; Bedani. Hao ndio wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase. Na dada yake, Hamolekethi, akamzaa Ish-hodu, na Abiezeri, na Mala. Na wana wa Shemida walikuwa Ahiani, na Shekemu, na Liki, na Aniamu. Na wana wa Efraimu; Shuthela, na mwanawe huyo ni Beredi, na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Ekada, na mwanawe huyo ni Tahathi; na mwanawe huyo ni Zabadi, na mwanawe huyo ni Shuthela; na Ezeri na Ekadi, ambao watu wa Gathi, wenyeji wa nchi, waliwaua, kwa sababu walishuka ili kuwapokonya ng'ombe wao. Na Efraimu, baba yao, akaomboleza siku nyingi, wakaja nduguze ili kumfariji. Naye akamwingilia mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana, akamwita jina lake Beria, kwa sababu maafa yalikuwa yameipata nyumba yake. Na binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga Beth-horoni, wa chini na wa juu, na Uzen-sheera. Mwanawe ni Refa, na Reshefu, na mwanawe huyo ni Tela, na mwanawe huyo ni Tahani; na mwanawe huyo ni Ladani, na mwanawe huyo ni Amihudi, na mwanawe huyo ni Elishama; na mwanawe huyo ni Nuni, na mwanawe huyo ni Yoshua. Na hizi ndizo miliki yao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake; na mipakani mwa wana wa Manase; Beth-sheani na vijiji vyake; na Taanaki na vijiji vyake; na Megido na vijiji vyake; na Dori na vijiji vyake. Katika miji hiyo walikaa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli. Wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na dada yao, Sera. Na wana wa Beria; Heberi, na Malkieli, aliyekuwa babaye Birzaithi. Na Heberi akamzaa Yafleti, na Shomeri, na Hothamu, na dada yao, Shua. Na wana wa Yafleti; Pasaki, na Bimhali, na Ashvathi. Hao ndio wana wa Yafleti. Na wana wa Shomeri; Ahi, na Roga, na Yehuba, na Aramu. Na wana wa nduguye Helemu; Sofa, na Imna, na Sheleshi, na Amali. Wana wa Sofa; Sua, na Harneferi, na Shuali, na Beri, na Imra; na Bezeri, na Hodu, na Shama, na Shilsha, na Ithrani, na Beera. Na wana wa Yetheri; Yefune, na Pispa, na Ara. Na wana wa Ula; Ara, na Hanieli na Risia. Hao wote ndio wana wa Asheri, wakuu wa koo za baba zao, watu wateule, hodari wa vita, viongozi wa wakuu. Na hesabu yao waliojumlishwa kwa vizazi vyao kwenda vitani walikuwa watu elfu ishirini na sita.
1 Mambo ya Nyakati 7:13-40 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yeseri, na Shilemu; wana wa Bilha. Wana wa Manase; Asrieli, ambaye suria yake, Mwarami, alimzalia, akamzalia na Makiri babaye Gileadi; naye Makiri akatwaa mke kwa Hupimu na Shupimu, ambao umbu lao aliitwa Maaka; na wa pili akaitwa jina lake Selofehadi; na Selofehadi alikuwa na binti. Na Maaka mkewe Makiri, akamzalia mwana, akamwita jina lake Pereshi; na jina la nduguye aliitwa Shereshi; na wanawe walikuwa Ulamu, na Rakemu. Na wana wa Ulamu; Bedani. Hao ndio wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase. Na umbu lake, Hamolekethi, akamzaa Ish-hodu, na Abiezeri, na Mala. Na wana wa Shemida walikuwa Ahiani, na Shekemu, na Liki, na Aniamu. Na wana wa Efraimu; Shuthela, na mwanawe huyo ni Beredi, na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Ekada, na mwanawe huyo ni Tahathi; na mwanawe huyo ni Zabadi, na mwanawe huyo ni Shuthela; na Ezeri na Ekadi, ambao watu wa Gathi, wenyeji wa nchi, waliwaua, kwa sababu walishuka ili kuzipokonya ng’ombe zao. Na Efraimu, baba yao, akaomboleza siku nyingi, wakaja nduguze ili kumfariji. Naye akamwingilia mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana, akamwita jina lake Beria, kwa sababu mna mabaya nyumbani mwake. Na binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga Beth-horoni, wa chini na wa juu, na Uzen-sheera. Mwanawe ni Refa, na Reshefu, na mwanawe huyo ni Tela, na mwanawe huyo ni Tahani; na mwanawe huyo ni Ladani, na mwanawe huyo ni Amihudi, na mwanawe huyo ni Elishama; na mwanawe huyo ni Nuni, na mwanawe huyo ni Yoshua. Na hizi ndizo hozi zao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake; na mipakani mwa wana wa Manase; Beth-sheani na vijiji vyake; na Taanaki na vijiji vyake; na Megido na vijiji vyake; na Dori na vijiji vyake. Katika miji hiyo walikaa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli. Wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na umbu lao, Sera. Na wana wa Beria; Heberi, na Malkieli, aliyekuwa babaye Birzaithi. Na Heberi akamzaa Yafleti, na Shomeri, na Hothamu, na umbu lao, Shua. Na wana wa Yafleti; Pasaki, na Bimhali, na Ashvathi. Hao ndio wana wa Yafleti. Na wana wa Shomeri; Ahi, na Roga, na Yehuba, na Aramu. Na wana wa nduguye Helemu; Sofa, na Imna, na Sheleshi, na Amali. Wana wa Sofa; Sua, na Harneferi, na Shuali, na Beri, na Imra; na Bezeri, na Hodu, na Shama, na Shilsha, na Ithrani, na Beera. Na wana wa Yetheri; Yefune, na Pispa, na Ara. Na wana wa Ula; Ara, na Hanieli na Risia. Hao wote ndio wana wa Asheri, wakuu wa mbari za baba zao, watu wateule, hodari wa vita, wakuu wa mashehe. Na hesabu yao waliojumlishwa kwa vizazi vyao kwenda vitani walikuwa watu ishirini na sita elfu.
1 Mambo ya Nyakati 7:13-40 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wana wa Naftali walikuwa: Yahzieli, Guni, Yeseri na Shalumu; hao walikuwa wazao wa Bilha. Wazao wa Manase walikuwa: Asirieli alikuwa mzao wake kutokana na suria wake Mwaramu. Huyu suria akamzaa Makiri baba wa Gileadi. Makiri akatwaa mke kutoka miongoni mwa Wahupimu na Washupimu. Jina la dada yake Makiri aliitwa Maaka. Mwana mwingine wa Makiri aliitwa Selofehadi, aliyekuwa na watoto wa kike tu. Maaka mkewe Makiri akamzaa mwana aliyemwita Pereshi. Jina la nduguye lilikuwa Shereshi. Wana wa Pereshi walikuwa Ulamu na Rakemu. Mwana wa Ulamu alikuwa: Bedani. Hao walikuwa wana wa Gileadi mwana wa Makiri, mwana wa Manase. Dada yake aliyeitwa Hamolekethi aliwazaa Ish-Hodi, Abiezeri na Mahla. Wana wa Shemida walikuwa: Ahiani, Shekemu, Liki na Aniamu. Wazao wa Efraimu walikuwa: Shuthela, ambaye alimzaa Beredi, Beredi akamzaa Tahathi, Tahathi akazaa Eleada, Eleada akamzaa Tahathi, Tahathi akamzaa Zabadi, na Zabadi akamzaa Shuthela. Ezeri na Eladi waliuawa na wenyeji wa Gathi walipokuwa wameenda huko kuwanyangʼanya mifugo yao. Baba yao Efraimu akawaombolezea kwa siku nyingi, na jamaa zake wakaja kumfariji. Kisha akakutana kimwili na mke wake tena, naye akachukua mimba, akamzalia mwana. Akamwita jina Beria, kwa sababu ya misiba iliyoipata nyumba yake. Beria alikuwa na binti jina lake Sheera. Huyu ndiye aliijenga miji ya Beth-Horoni ya Juu na Beth-Horoni ya Chini, pamoja na Uzen-Sheera. Beria akamzaa pia Refa, naye Refa akamzaa Reshefu, Reshefu akamzaa Tela, Tela akamzaa Tahani, Tahani akamzaa Ladani, Ladani akamzaa Amihudi, Amihudi akamzaa Elishama, Elishama akamzaa Nuni, Nuni akamzaa Yoshua. Nchi zao na makazi yao yalijumuisha Betheli na vijiji vilivyouzunguka, Naarani ilikuwa upande wa mashariki, Gezeri pamoja na vijiji vyake upande wa magharibi, pia Shekemu na vijiji vyake hadi kufikia Aya na vijiji vyake. Katika mipaka ya Manase kulikuwa na Beth-Shani, Taanaki, Megido na Dori pamoja na vijiji vyake. Wazao wa Yusufu mwana wa Israeli waliishi katika miji hii. Wana wa Asheri walikuwa: Imna, Ishva, Ishvi na Beria. Dada yao alikuwa Sera. Wana wa Beria walikuwa: Heberi na Malkieli, aliyekuwa baba yake Birzaithi. Heberi akawazaa Yafleti, Shomeri na Hothamu, na Shua dada yao. Wana wa Yafleti walikuwa: Pasaki, Bimhali na Ashvathi. Hawa walikuwa wana wa Yafleti. Wana wa Shemeri walikuwa: Ahi, Roga, Yehuba na Aramu. Wana wa Helemu ndugu yake walikuwa: Sofa, Imna, Sheleshi na Amali. Wana wa Sofa walikuwa: Sua, Harneferi, Shuali, Beri, Imra, Bezeri, Hodu, Shama, Shilsha, Ithrani na Beera. Wana wa Yetheri walikuwa: Yefune, Pispa na Ara. Wana wa Ula walikuwa: Ara, Hanieli na Risia. Hawa wote ndio walikuwa wazao wa Asheri, viongozi wa jamaa zao, watu bora, mashujaa hodari na viongozi maarufu. Idadi ya watu waliokuwa wamejiandaa kwa vita, kama walivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa elfu ishirini na sita.