1 Mambo ya Nyakati 7:1-5
1 Mambo ya Nyakati 7:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Wana wa Isakari walikuwa wanne: Tala, Pua, Yashubu na Shimroni. Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaya, Yerieli, Yamai, Ibsamu na Shemueli. Hao walikuwa wakuu wa jamaa za koo za Tola na watu mashujaa sana wa vita nyakati zao. Idadi ya wazawa wao siku za mfalme Daudi ilikuwa 22,600. Uzi alikuwa na mwana mmoja, jina lake Izrahia. Na wana wa Izrahia walikuwa Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia, jumla wanne, na wote walikuwa wakuu wa jamaa. Kwa vile ambavyo wake na watoto wao walikuwa wengi sana, mliweza kupatikana vikosi vya wanajeshi 36,000 kutokana na wazawa wao. Ndugu zao katika jamaa zote za kabila la Isakari walioandikishwa kwa kufuata koo, walikuwa 87,000, na wote walikuwa mashujaa wa vita.
1 Mambo ya Nyakati 7:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na wana wa Isakari; Tola, na Puva, na Yashubu, na Shimroni, wanne. Na wana wa Tola; Uzi, na Refaya, na Yerieli, na Yamai, na Ibsamu, na Shemueli, wakuu wa koo za baba zao, yaani, wa Tola; watu hodari wa vita katika vizazi vyao; hesabu yao katika siku za Daudi ilikuwa watu elfu ishirini na mbili na mia sita. Na wana wa Uzi; Izrahia; na wana wa Izrahia; Mikaeli, na Obadia, na Yoeli, na Ishia, watano; wote wakuu. Na pamoja nao, katika vizazi vyao, kulingana na koo za baba zao, walikuwapo vikosi vya jeshi la vita, watu elfu thelathini na sita; kwa kuwa wake zao na watoto wao walikuwa wengi. Na ndugu zao katika jamaa zote za Isakari, watu hodari wa vita, wakihesabiwa kwa vizazi vyao, walikuwa watu elfu themanini na saba.
1 Mambo ya Nyakati 7:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na wana wa Isakari; Tola, na Puva, na Yashubu, na Shimroni, wanne. Na wana wa Tola; Uzi, na Refaya, na Yerieli, na Yamai, na Ibsamu, na Shemueli, wakuu wa mbari za baba zao, yaani, wa Tola; watu hodari wa vita katika vizazi vyao; hesabu yao katika siku za Daudi ilikuwa watu ishirini na mbili elfu na mia sita. Na wana wa Uzi; Izrahia; na wana wa Izrahia; Mikaeli, na Obadia, na Yoeli, na Ishia, watano; wote wakuu. Na pamoja nao, katika vizazi vyao, sawasawa na mbari za baba zao, walikuwapo vikosi vya jeshi la vita, watu thelathini na sita elfu; kwa kuwa wake zao na watoto wao walikuwa wengi. Na ndugu zao katika jamaa zote za Isakari, watu hodari wa vita, wakihesabiwa kwa vizazi vyao, walikuwa watu themanini na saba elfu.
1 Mambo ya Nyakati 7:1-5 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Wana wa Isakari walikuwa: Tola, Pua, Yashubu na Shimroni; wote ni wanne. Wana wa Tola walikuwa: Uzi, Refaya, Yerieli, Yahmai, Ibsamu na Samweli waliokuwa viongozi wa jamaa zao. Wakati wa utawala wa Mfalme Daudi, wazao wa Tola walioorodheshwa kama wapiganaji katika ukoo wao walikuwa watu elfu ishirini na mbili na mia sita. Mwana wa Uzi alikuwa: Izrahia. Wana wa Izrahia walikuwa: Mikaeli, Obadia, Yoeli na Ishia. Wote hawa watano walikuwa wakuu wao. Kulingana na ukoo wa jamaa zao, walikuwa na watu elfu thelathini na sita waliokuwa wamejiandaa kwa vita, kwa sababu walikuwa na wanawake na watoto wengi. Jamaa waliokuwa wapiganaji kutoka koo zote za Isakari, kama walivyoorodheshwa katika ukoo wao, walikuwa elfu themanini na saba.