1 Mambo ya Nyakati 21:13-14
1 Mambo ya Nyakati 21:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Daudi akamjibu Gadi, “Nimeingia katika mashaka makubwa! Lakini afadhali niadhibiwe na Mwenyezi-Mungu kwani yeye ana huruma sana. Ila nisianguke katika mkono wa mwanadamu.” Basi, Mwenyezi-Mungu akawaletea Waisraeli maradhi mabaya, ambayo yalisababisha vifo vya Waisraeli 70,000.
1 Mambo ya Nyakati 21:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na nianguke katika mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema zake ni nyingi sana; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu. Basi BWANA akawaletea Israeli tauni; nao wakaanguka wa Israeli watu elfu sabini.
1 Mambo ya Nyakati 21:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Naye Daudi akamwambia Gadi, Nimeingia katika mashaka sana; basi sasa na nianguke katika mkono wa BWANA; kwa kuwa rehema zake ni nyingi sana; wala nisianguke katika mkono wa wanadamu. Basi BWANA akawaletea Israeli tauni; nao wakaanguka wa Israeli watu sabini elfu.
1 Mambo ya Nyakati 21:13-14 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Daudi akamwambia Gadi, “Ninayo mahangaiko makubwa. Mimi na nianguke mikononi mwa BWANA, kwa maana rehema zake ni kuu mno, lakini usiniache niangukie mikononi mwa wanadamu.” Basi BWANA akatuma tauni katika Israeli, na wanaume elfu sabini wa Israeli wakafa.