1 Mambo ya Nyakati 20:6
1 Mambo ya Nyakati 20:6 Biblia Habari Njema (BHN)
Baadaye kulitokea tena vita huko Gathi ambako kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na kimo kikubwa, na vidole sita katika kila mkono, na vidole sita katika kila mguu, jumla yake vidole ishirini na vinne. Yeye pia alikuwa mzawa wa majitu.
1 Mambo ya Nyakati 20:6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambapo palikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole vya mikono na miguu ishirini na vinne, kila mguu sita, na kila mkono sita; naye alizaliwa na Mrefai.
1 Mambo ya Nyakati 20:6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambapo palikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole vya mikono na miguu ishirini na vinne, kila mguu sita, na kila mkono sita; naye alizaliwa na Mrefai.
1 Mambo ya Nyakati 20:6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Katika vita vingine tena, vilivyopiganwa huko Gathi, kulikuwa na mtu mmoja mkubwa, mwenye vidole sita katika kila mkono, na vidole sita katika kila mguu: jumla vidole ishirini na vinne. Yeye alikuwa pia mzao wa Mrefai.