1 Mambo ya Nyakati 20:4-8
1 Mambo ya Nyakati 20:4-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Baada ya hayo, kulitokea vita na Wafilisti huko Gezeri. Sibekai, Mhushathi, akamuua Sipai aliyekuwa mmojawapo wa wazawa wa Warefai; hivyo Wafilisti wakawa wameshindwa. Kulitokea tena vita na Wafilisti. Naye Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mpini wa mkuki wake, ulikuwa kama mti wa mfumaji. Baadaye kulitokea tena vita huko Gathi ambako kulikuwa na mtu mmoja aliyekuwa na kimo kikubwa, na vidole sita katika kila mkono, na vidole sita katika kila mguu, jumla yake vidole ishirini na vinne. Yeye pia alikuwa mzawa wa majitu. Naye alipowatukana Waisraeli, Yonathani, mwana wa Shimea, nduguye Daudi, alimuua. Hao walikuwa wazawa wa majitu huko Gathi; nao waliuawa na Daudi pamoja na watumishi wake.
1 Mambo ya Nyakati 20:4-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikawa baada ya hayo, kulitokea vita na Wafilisti huko Gezeri; ndipo Sibekai, Mhushathi, alipomwua Safu, mmojawapo wa Warefai; nao Wafilisti wakashindwa. Kulikuwa na vita tena na Wafilisti; na Elhanani, mwana wa Yairi akamwua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mti wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji. Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambapo palikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole vya mikono na miguu ishirini na vinne, kila mguu sita, na kila mkono sita; naye alizaliwa na Mrefai. Naye huyo alipowatukana Israeli, Yonathani, mwana wa Shama, nduguye Daudi, akamwua. Hao walizaliwa kwake huyo Mrefai wa Gathi, nao wakaanguka kwa mkono wa Daudi, na kwa mkono wa watumishi wake.
1 Mambo ya Nyakati 20:4-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa baada ya hayo, kulitokea vita na Wafilisti huko Gobu; ndipo Sibekai, Mhushathi, alipomwua Safu, mmojawapo wa Warefai; nao wakashindwa. Kulikuwa na vita tena na Wafilisti; na Elhanani, mwana wa Yairi akamwua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mti wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji. Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambapo palikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole vya mikono na miguu ishirini na vinne, kila mguu sita, na kila mkono sita; naye alizaliwa na Mrefai. Naye huyo alipowatukana Israeli, Yonathani, mwana wa Shama, nduguye Daudi, akamwua. Hao walizaliwa kwake huyo Mrefai wa Gathi, nao wakaanguka kwa mkono wa Daudi, na kwa mkono wa watumishi wake.
1 Mambo ya Nyakati 20:4-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Baada ya muda, kulitokea vita dhidi ya Wafilisti, huko Gezeri. Wakati huo Sibekai, Mhushathi, akamuua Sipai, aliyekuwa mmoja wa wazao wa Warefai, nao Wafilisti wakashindwa. Katika vita vingine na Wafilisti, Elhanani mwana wa Yairi alimuua Lahmi nduguye Goliathi, Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa na mpini kama mti wa mfumaji. Katika vita vingine tena, vilivyopiganwa huko Gathi, kulikuwa na mtu mmoja mkubwa, mwenye vidole sita katika kila mkono, na vidole sita katika kila mguu: jumla vidole ishirini na vinne. Yeye alikuwa pia mzao wa Mrefai. Alipowadhihaki Israeli, Yonathani, mwana wa Shimea, nduguye Daudi, akamuua. Hao walikuwa wazao wa Warefai huko Gathi, nao walianguka kwa mikono ya Daudi na watu wake.