Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

1 Mambo ya Nyakati 1:1-54

1 Mambo ya Nyakati 1:1-54 Biblia Habari Njema (BHN)

Adamu alimzaa Sethi, Sethi akamzaa Enoshi, Enoshi akamzaa Kenani, Kenani akamzaa Mahalaleli, Mahalaleli akamzaa Yaredi, Yaredi akamzaa Henoki, Henoki akamzaa Methusela. Methusela alimzaa Lameki, Lameki akamzaa Noa. Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi. Wana wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. Wana wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Difathi na Togama. Wana wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misri, Puti na Kanaani. Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani. Kushi alimzaa Nimrodi, aliyekuwa mtu shujaa wa kwanza duniani. Wazawa wa Misri ni Waludi, Waanamu, Walehabi, Wanaftuhi, Wapathrusi Wakaftori na Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti). Wana wa Kanaani walikuwa Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi. Kanaani pia ndiye babu yao Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, Wahivi, Waarki, Wasini, Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuri, Arpaksadi, Ludi, Aramu, Usi, Huli, Getheri na Mesheki. Arpaksadi alimzaa Shela, Shela akamzaa Eberi. Eberi alikuwa na wana wawili; mmoja wao aliitwa Pelegi, (kwa maana wakati wake watu walikuwa wametawanyika duniani), na ndugu yake aliitwa Yoktani. Wana wa Yoktani walikuwa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, Hadoramu, Uzali, Dikla, Obali, Abimaeli, Sheba, Ofiri, Havila na Yobabu. Hao watu ni wana wa Yoktani. Ukoo wa Abrahamu kutokea Shemu ni kama ifuatavyo: Shemu alimzaa Arpaksadi, naye Arpaksadi akamzaa Shela. Shela akamzaa Eberi, Eberi akamzaa Pelegi, Pelegi akamzaa Reu; Reu akamzaa Serugi, Serugi akamzaa Nahori, Nahori akamzaa Tera, na Tera akamzaa Abramu, ambaye ndiye Abrahamu. Abrahamu alikuwa na watoto wawili wa kiume: Isaka na Ishmaeli. Hivi ndivyo vizazi vyao: Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli alikuwa Nebayothi na wengine ni Kedari, Adbeeli, Mibsamu, Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli. Abrahamu alikuwa na suria aliyeitwa Ketura. Ketura alimzalia Abrahamu: Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa Sheba na Dedani. Wana wa Midiani walikuwa: Efa, Eferi, Henoki, Abida na Eldaa. Wote hao walikuwa wazawa wa Ketura. Isaka, mwana wa Abrahamu, alikuwa na wana wawili: Esau na Israeli. Wana wa Esau walikuwa Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora. Wana wa Elifazi walikuwa Temani, Omari, Sefo, Gatamu, Kenazi, Timna na Amaleki. Wana wa Reueli walikuwa Nahathi, Zera, Shama na Miza. Wana wa Seiri walikuwa Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani. Wana wa Lotani walikuwa wawili: Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna. Wana wa Shobali walikuwa Alvani, Manahathi, Ebali, Shefi na Onamu. Wana wa Sibeoni walikuwa Aya na Ana. Mwana wa Ana alikuwa Dishoni; na wana wa Dishoni walikuwa Hamrani, Eshbani, Ithrani na Kerani. Wana wa Eseri walikuwa Bilhani, Zaawani na Akani; na wana wa Dishoni walikuwa Usi na Arani. Wafuatao ndio wafalme waliotawala nchi ya Edomu kabla mfalme yeyote hajatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori alitawala nchi ya Edomu, akiwa na makao yake makuu katika mji wa Dinhaba. Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra alitawala badala yake. Yobabu alipofariki, Hushamu wa nchi ya Watemi alitawala badala yake. Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi alitawala badala yake, makao yake makuu yakiwa katika mji wa Avithi. Huyu ndiye aliyewapiga na kuwashinda Wamidiani katika nchi ya Moabu. Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka alitawala badala yake. Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ulio karibu na mto Eufrate, alitawala badala yake. Shauli alipofariki, Baal-hanani mwana wa Akbori alitawala badala yake. Baal-hanani alipofariki, Hadadi kutoka Pai alitawala badala yake na jina la mkewe Akbori lilikuwa Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. Naye Hadadi akafariki. Wakuu wa makabila ya Edomu walikuwa Timna, Alva, Yethethi, Oholibama, Ela, Pinoni, Kenazi, Temani, Mibsari, Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.

1 Mambo ya Nyakati 1:1-54 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Adamu, na Sethi, na Enoshi; na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi; na Henoko, na Methusela, na Lameki; na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi. Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani. Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani. Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi, na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori. Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi; na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi; na Mhivi, na Mwarki, na Msini; na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi. Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani. Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera; na Hadoramu, na Uzali, na Dikla; na Obali, na Abimaeli, na Sheba; na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani. Shemu, na Arfaksadi, na Sala; na Eberi, na Pelegi, na Reu; na Serugi, na Nahori, na Tera; na Abramu, naye ndiye Abrahamu. Wana wa Abrahamu; Isaka, na Ishmaeli. Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu; na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema; na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli. Na wana wa Ketura, suria yake Abrahamu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani. Na wana wa Midiani; Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote ndio wana wa Ketura. Na Abrahamu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli. Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora. Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki. Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza. Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani. Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni dada yake Lotani. Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana. Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani. Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani. Basi hawa ndio wafalme waliotawala katika nchi ya Edomu, kabla hajatawala mfalme yeyote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba. Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akatawala badala yake. Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akatawala badala yake. Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akatawala badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi. Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akatawala badala yake. Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akatawala badala yake. Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akatawala badala yake. Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akatawala badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi; na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni; na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari; na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu.

1 Mambo ya Nyakati 1:1-54 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Adamu, na Sethi, na Enoshi; na Kenani, na Mahalaleli, na Yaredi; na Henoko, na Methusela, na Lameki; na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi. Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi. Na wana wa Gomeri; Ashkenazi, na Rifathi, na Togama. Na wana wa Yavani; Elisha, na Tarshishi, na Kitimu, na Warodani. Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani. Na wana wa Kushi; Seba, na Havila, na Sabta, na Raama, na Sabteka. Na wana wa Raama; Sheba, na Dedani. Kushi naye akamzaa Nimrodi; yeye akaanza kuwa mtu hodari katika nchi. Na Misri akazaa Waludi, na Waanami, na Walehabi, na Wanaftuhi, na Wapathrusi, na Wakasluhi; huko ndiko walikotoka Wafilisti, na Wakaftori. Na Kanaani akamzaa Sidoni, mwanawe wa kwanza, na Hethi; na Myebusi, na Mwamori, na Mgirgashi; na Mhivi, na Mwarki, na Msini; na Mwarvadi, na Msemari, na Mhamathi. Wana wa Shemu; Elamu, na Ashuru, na Arfaksadi, na Ludi, na Aramu, na Usi, na Huli, na Getheri, na Mashi. Na Arfaksadi akamzaa Sala, na Sala akamzaa Eberi. Na Eberi akazaliwa wana wawili wa kiume; jina la wa kwanza aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika; na jina la nduguye aliitwa Yoktani. Na Yoktani akamzaa Almodadi, na Shelefu, na Hasarmawethi, na Yera; na Hadoramu, na Uzali, na Dikla; na Obali, na Abimaeli, na Sheba; na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani. Shemu, na Arfaksadi, na Sala; na Eberi, na Pelegi, na Reu; na Serugi, na Nahori, na Tera; na Abramu, naye ndiye Ibrahimu. Wana wa Ibrahimu; Isaka, na Ishmaeli. Hivi ndivyo vizazi vyao; mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, Nebayothi; kisha Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu; na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema; na Yeturi, na, Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli. Na wana wa Ketura, suria yake Ibrahimu; yeye akamzaa Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Shua. Na wana wa Yokshani; Sheba na Dedani. Na wana wa Midiani; Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote ndio wana wa Ketura. Na Ibrahimu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli. Wana wa Esau; Elifazi, na Reueli, na Yeushi, na Yalamu, na Kora. Wana wa Elifazi; Temani, na Omari, na Sefo, na Gatamu, na Kenazi, na, kwa Timna, Amaleki. Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza. Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani. Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni umbu lake Lotani. Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana. Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani. Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani. Basi hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla hajamiliki mfalme awaye yote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba. Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akamiliki badala yake. Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akamiliki badala yake. Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akamiliki badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi. Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akamiliki badala yake. Samla akafa, naye Shauli, wa Rehobothi karibu na Mto, akamiliki badala yake. Shauli akafa, naye Baal-Hanani, mwana wa Akbori, akamiliki badala yake. Baal-Hanani akafa, naye Hadadi akamiliki badala yake; na jina la mji wake ni Pau; na jina la mkewe ni Mehetabeli, binti Matredi, binti Mezahabu. Akafa Hadadi. Na hawa ndio majumbe wa Edomu; jumbe Timna, na jumbe Alva, na jumbe Yethethi; na jumbe Oholibama, na jumbe Ela, na jumbe Pinoni; na jumbe Kenazi, na jumbe Temani, na jumbe Mibsari; na jumbe Magdieli, na jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu.

1 Mambo ya Nyakati 1:1-54 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)

Adamu, Sethi, Enoshi, Kenani, Mahalaleli, Yaredi, Henoko, Methusela, Lameki, Nuhu. Wana wa Nuhu walikuwa: Shemu, Hamu na Yafethi. Wana wa Yafethi walikuwa: Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki na Tirasi. Wana wa Gomeri walikuwa: Ashkenazi, Rifathi na Togarma. Wana wa Yavani walikuwa: Elisha, Tarshishi, Kitimu na Rodanimu. Wana wa Hamu walikuwa: Kushi, Misri, Putu na Kanaani. Wana wa Kushi walikuwa: Seba, Havila, Sabta, Raama na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa: Sheba na Dedani. Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikua shujaa mwenye nguvu duniani. Misri akawazaa: Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi, Wapathrusi, Wakasluhi (hao ndio asili ya Wafilisti) na Wakaftori. Wana wa Kanaani walikuwa: Sidoni, mzaliwa wake wa kwanza, na Hethi, Wayebusi, Waamori, Wagirgashi, Wahivi, Waarki, Wasini, Waarvadi, Wasemari na Wahamathi. Wana wa Shemu walikuwa: Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi na Aramu. Wana wa Aramu walikuwa: Usi, Huli, Getheri na Mashi. Arfaksadi akamzaa Shela, Shela akamzaa Eberi. Eberi alipata wana wawili: Mmoja wao aliitwa Pelegi, kwa kuwa wakati wake dunia iligawanyika; nduguye aliitwa Yoktani. Wana wa Yoktani walikuwa: Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera, Hadoramu, Uzali, Dikla, Obali, Abimaeli, Sheba, Ofiri, Havila na Yobabu. Wote hawa walikuwa wana wa Yoktani. Wana wa Shemu walikuwa Arfaksadi, Shela, Eberi, Pelegi, Reu, Serugi, Nahori, Tera, Tera akamzaa Abramu (yaani Abrahamu). Abrahamu alikuwa na wana wawili: Isaka na Ishmaeli. Hawa ndio wazao wao: Ishmaeli akazaa Nebayothi mzaliwa wa kwanza; kisha Kedari, Adbeeli, Mibsamu, Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli. Wana waliozaliwa na Ketura suria wa Abrahamu walikuwa: Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa: Sheba na Dedani. Wana wa Midiani walikuwa: Efa, Eferi, Hanoki, Abida na Eldaa. Wote hao walikuwa wa uzao wa Ketura. Abrahamu alikuwa baba wa Isaka. Wana wa Isaka walikuwa: Esau na Israeli. Wana wa Esau walikuwa: Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu na Kora. Wana wa Elifazi walikuwa: Temani, Omari, Sefo, Gatamu na Kenazi; Elifazi kwa Timna akamzaa Amaleki. Wana wa Reueli walikuwa: Nahathi, Zera, Shama na Miza. Wana wa Seiri walikuwa: Lotani, Shobali, Sibeoni, Ana, Dishoni, Eseri na Dishani. Wana wa Lotani walikuwa wawili: Hori na Homamu. Lotani alikuwa na dada yake aliyeitwa Timna. Wana wa Shobali walikuwa: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo na Onamu. Wana wa Sibeoni walikuwa: Aya na Ana. Mwana wa Ana alikuwa: Dishoni. Nao wana wa Dishoni walikuwa: Hemdani, Eshbani, Ithrani na Kerani. Wana wa Eseri walikuwa: Bilhani, Zaavani na Akani. Wana wa Dishani walikuwa: Usi na Arani. Hawa ndio wafalme waliotawala Edomu kabla hajatawala mfalme yeyote wa Waisraeli: Bela mwana wa Beori, ambaye mji wake ni Dinhaba. Bela alipofariki, Yobabu mwana wa Zera kutoka Bosra akawa mfalme baada yake. Yobabu alipofariki, Hushamu kutoka nchi ya Watemani akawa mfalme baada yake. Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi, aliyeshinda Midiani katika nchi ya Moabu, akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Avithi. Hadadi alipofariki, Samla kutoka Masreka akawa mfalme baada yake. Samla alipofariki, Shauli kutoka Rehobothi ngʼambo ya Mto Frati, akawa mfalme baada yake. Shauli alipofariki, Baal-Hanani mwana wa Akbori akawa mfalme baada yake. Baal-Hanani alipofariki, Hadadi akawa mfalme baada yake. Mji wake uliitwa Pau, na mkewe aliitwa Mehetabeli binti Matredi, binti Me-Zahabu. Naye Hadadi pia akafa. Wakuu wa Edomu walikuwa: Timna, Alva, Yethethi, Oholibama, Ela, Pinoni, Kenazi, Temani, Mibsari, Magdieli na Iramu. Hao ndio wakuu wa makabila ya Edomu.