Zaburi 41:7-10
Zaburi 41:7-10 BHN
Wote wanichukiao hunongonezana juu yangu; wananiwazia mabaya ya kunidhuru. Husema: “Maradhi haya yatamuua; hatatoka tena kitandani mwake!” Hata rafiki yangu wa moyoni niliyemwamini, rafiki ambaye alishiriki chakula changu, amegeuka kunishambulia! Ee Mwenyezi-Mungu, unionee huruma! Unipe nafuu, nami nitawalipiza.