Kisha akawaambia mfano: “Angalieni mtini na miti mingine yote. Mnapoona kwamba imeanza kuchipua majani, mwatambua kwamba majira ya mavuno yamekaribia. Vivyo hivyo, mtakapoona mambo hayo yanatendeka, mtatambua kwamba ufalme wa Mungu umekaribia. Kweli nawaambieni, kizazi hiki cha sasa hakitapita kabla ya hayo yote kutendeka. Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe. “Muwe macho, mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na shughuli za maisha haya. La sivyo, siku ile itawajieni ghafla. Kwa maana itawajia kama mtego wote wanaoishi duniani pote. Muwe waangalifu basi, na salini daima ili muweze kupata nguvu ya kupita salama katika mambo haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele ya Mwana wa Mtu.” Wakati wa mchana, siku hizo, Yesu alikuwa akifundisha watu hekaluni; lakini usiku alikuwa akienda katika mlima wa Mizeituni na kukaa huko. Watu wote walikuwa wanakwenda hekaluni asubuhi na mapema, wapate kumsikiliza.
Soma Luka 21
Sikiliza Luka 21
Shirikisha
linganisha matoleo yote: Luka 21:29-38
Hifadhi mistari, soma bila mtandao, tazama klipu za mafunzo, na zaidi!
YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha
Nyumbani
Biblia
Mipango
Video