Waroma 10
10
Wayuda waliukataa wongofu wa Mungu.
1*Ndugu, moyo wangu unayapenda sana, ninayomwomba Mungu kwamba: Waisiraeli waokoke. 2Kwani nawashuhudia, ya kuwa waona wivu kwa ajili yake Mungu, lakini hawamtambui. 3Kwani wongofu, Mungu anaoutaka, hawaujui, wakajaribu kujiongoza wenyewe, lakini hivyo hawakuutii ule wongofu, Mungu anaoutaka.#Rom. 9:31-32. 4Kwani timilizo la Maonyo ni Kristo, kila mwenye kumtegemea ajipatie wongofu!#Mat. 5:17; Yoh. 1:17; 3:18; Gal. 3:24-25; Ebr. 8:13. 5Kwani Mose aliandika:
Anayeufanya wongofu ulioagizwa na Maonyo
mtu huyo atapata uzima kwa njia hiyo.#3 Mose 18:5.
6Lakini wongofu unaopatikana kwa kumtegemea Mungu unasema hivyo: Usiseme moyoni mwako: Yuko nani atakayepaa kwenda mbinguni? Huko ndiko kumshusha Kristo.#5 Mose 30:12-13. 7Wala usiseme: Yuko nani atakayeshuka kwenda kuzimuni? Huko ndiko kumpaza Kristo na kumtoa kwenye wafu. 8Tena unasema:
Neno hilo linakukalia karibu, limo kinywani mwako,
namo moyoni mwako.
Hilo ndilo neno la kumtegemea Mungu, ni hilihili, tunalolitangaza.#5 Mose 30:14. 9Kwani ukiungama kwa kinywa chako kwamba: BWANA NI YESU, ukamtegemea kwa moyo wako kwamba: Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka.#2 Kor. 4:5. 10Kwani ukimtegemea kwa moyo unapata wongofu; ukimwungama kwa kinywa unaokoka. 11Kwani Maandiko yasema: Kila anayemtegemea hatatwezeka.#Yes. 28:16. 12Kwani hapa hawachaguliwi Wayuda na Wagriki; kwani aliye Bwana wao wote ni yuyu huyu mmoja, ni mwenye magawio yanayowatoshea wote wanaomtambikia.#Tume. 10:34; 15:9. 13Kwani;
Kila atakayelitambikia Jina la Bwana ataokoka.#Yoe. 2:32. 14Basi, watamtambikiaje, wasiyemtegemea? Tena watamtegemeaje, ambaye hawajamsikia Neno lake? Tena watasikiaje, pasipokuwapo mwenye kutangaza? 15Tena watatangazaje, wasipotumwa? Ndivyo ilivyoandikwa:
Tazameni, miguu yao wapiga mbiu njema jinsi inavyopendeza!*#Yes. 52:7. 16Lakini walioutii huo Utume mwema sio wote. Kwani Yesaya anasema:
Bwana, yuko nani anayeutegemea utume wetu?#Yes. 53:1. 17Basi, kumtegemea Mungu huletwa na matangazo, lakini matangazo hutoka katika Neno la Kristo.#Yoh. 17:20. 18Lakini niseme: Hawakusikia? Kusikia wamesikia.
Uvumi wao ulitokea katika nchi zote;
nayo maneno yao yalifika hata mapeoni kwa ulimwengu.#Rom. 15:19; Sh. 19:5. 19Au niseme: Waisiraeli hawakulitambua? Kwanza Mose anasema:
Mimi na niwachokoze ninyi nikiwaletea watu wasio watu,
na niwakasirishe ninyi nikiwaletea taifa la watu
wasiojua maana.#5 Mose 32:21. 20Kisha Yesaya anajipa moyo wa kusema:
Nimeonwa nao wasionitafuta, nikawatokea wasioniuliza.#Yes. 65:1. 21Lakini Waisiraeli anawaambia:
Mchana kutwa naliikunjua mikono yangu,
nipungie ukoo wa watu wasioonyeka, walio wabishi tu.#Yes. 65:2.
Iliyochaguliwa sasa
Waroma 10: SRB37
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.

: