Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Malaki 4

4
Siku ya Bwana.
1*Kwani mtaiona hiyo siku, ikija na kuwaka moto kama wa tanuru; ndipo, waliomsahau Mungu nao wote waliofanya maovu watakapokuwa makapi, siku hiyo ijayo itakapoyateketeza, isisaze wala mizizi wala matawi yao hao; ndivyo, Bwana Mwenye vikosi anavyosema. 2Lakini ninyi mliogopao Jina langu jua la wongofu litawachea, nalo litakuwa linao uponya mabawani mwake; ndipo, mtakapochezacheza kama ndama watokao zizini.#Luk. 1:78. 3Nao wasiomcha Bwana mtawaponda na kuwakanyagakanyaga, kwani watageuka kuwa uvumbi chini ya nyayo za miguu yenu siku hiyo, nitakayoifanya mimi.#Mal. 3:17.
4Yakumbukeni Maonyo ya mtumishi wangu Mose, niliyomwagiza kule Horebu, awafundishe Waisiraeli wote maongozi na maagizo. 5Na mwone, nikimtuma mfumbuaji Elia kuja kwenu, siku kubwa ya Bwana iogopeshayo itakapokuwa haijatimia bado.#Yoe. 3:4; Mat. 11:14; 17:11-13. 6Yeye ndiye atakayeigeuza mioyo ya baba, warudi kwa watoto, nayo ya watoto, warudi kwa baba zao, nisije kuipiga nchi na kuiapiza.*#Luk. 1:17.

Iliyochaguliwa sasa

Malaki 4: SRB37

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia